SIMBA WAMEANZA KUTESEKA MAPEMA

DUDE lililowakosesha ubingwa Simba chini ya Kocha Mkuu Roberto Oliveira la kukwama kupata matokeo kwenye mechi za ugenini limeanza kuitesa timu hiyo mapema kabla ligi kuanza.

Ipo wazi kuwa msimu wa 2022/23 ni Yanga ilitwaa ubingwa ilipokomba pointi 78 katika mechi 15 za ugenini ilishinda mechi 12, kichapo mechi mbili na sare ya bila kufungana ilikuwa moja ambapo walivuna pointi 37 ugenini na safu ya ushambuliaji ilitupia mabao 25.SIMBAWatani wao wa jadi, Simba kwenye mechi 15 walizocheza ugenini walikomba ushindi mechi 9 na waliambulia sare mechi tano na walitunguliwa mechi moja na kukusanya pointi 32 ugenini ikagotea nafasi ya pili kwenye ligi na pointi zake 73.

Tofauti ya Yanga na Simba kwenye pointi ilikuwa ni pointi tano ambapo Simba ilipoteza pointi nyingi zaidi ugenini huku Yanga wakiwapoteza hapo walipokomba pointi nyingi zilizowatenganisha na mstari wao wa kutwaa ubingwa.

Wakati ligi inaanza Simba imekuwa kwenye wakati mgumu kupata ushindi ugenini ilipoanza katika mechi za Ngao ya Jamii ambapo kwenye mechi mbili haijapata ushindi ndani ya dakika 90 mechi zote zilizochezwa Uwanja wa Mkwakwani.DUDE lililowakosesha ubingwa Simba chini ya Kocha Mkuu Roberto Oliveira la kukwama kupata matokeo kwenye mechi za ugenini limeanza kuitesa timu hiyo mapema kabla ligi kuanza.Licha ya Simba kutwaa taji la Ngao ya Jamii ushindi walipata kwa changamoto ya penalti kila hatua kuanzia nusu fainali dhidi ya Singida Fountain Gate (4-2) na fainali dhidi ya Yanga (1-3).

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.