SKUDU MAMBO FRESH YANGU

TAARIFA njema kwa mashabiki wa Yanga ni juu ya kupona kwa winga wao, Skudu Mahlatse Makudubela ambaye alikumbwa na majeraha jambo ambalo mashabiki wengi walishindwa kumfaidi winga huyo baada ya msimu kuanza rasmi.

Makudubela mara ya mwisho kuonekana uwanjani ilikuwa katika mchezo wa Ngao ya jamii dhidi ya Azam FC Tanga, ambapo katika mchezo huo alishindwa kuumaliza baada ya kuumia dakika ya tano tu ya mchezo.YANGAWinga huyo raia wa Afrika Kusini huu ni msimu wake wa kwanza ndani ya Yanga baada ya kusajiliwa akitokea katika Klabu ya Marumo Gallants ambayo ilishuka daraja katika ligi hiyo msimu uliopita.

Tayari,Skudu Makudubela amefanikiwa kuanza kucheza mechi za kirafiki na juzi Jumamosi alionekana uwanjani kipindi cha pili alipoingia kucheza katika mchezo wa kirafiki ambao Yanga walicheza dhidi ya Kiluvya na kuibuka na ushindi wa mabao 6-0.skuduKatika mchezo huo, winga Skudu alionekana akiingia kipindi cha pili akichukua nafasi ya Farrid Mussa jambo ambalo ni furaha kwa mashabiki wa Yanga kwani kuanza kucheza kwa winga huyo inaonyesha dalili njema kuelekea katika michezo yao miwili ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Merreikh

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.