Simba Yabanwa Mbavu Zambia

Klabu ya soka ya Simba imebanwa mbavu nchini Zambia katika mchezo wa kuwania kufuzu hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa barani Afrika baada ya kulazimishwa sare.

Simba ambayo ilikua ugenini kukipiga na klabu ya Power Dynamos ya nchini Zambia ililazimishwa sare na klabu hiyo ya mabao mawili kwa mawili, Huku klabu hiyo kutoka mitaa ya Msimbazi wakisawazisha bao jioni kabisa.simbaWekundu wa Msimbazi walionekana kuingia katika mchezo huo kwa tahadhari kubwa hasa kipindi cha kwanza ambapo waliipa nafasi klabu ya Power Dynamos kufika mara kwa mara katika lango lao na kufikanikiwa kupata bao kipindi cha kwanza.

Kipindi cha pili wekundu wa Msimbazi walionekana kuja kwa kasi na kuhitaji kusawazisha bao ambalo walikua wametanguliwa kipindi cha kwanza na walifanikiwa, Kwani kiungo wa klabu hiyo Clatous Chama aliwarudisha mchezoni.simbaDakika ya 75 ya mchezo Power Dynamos walifanya shambulio la kushtukiza na mshambuliaji Mulombwa kuipatia bao la pili klabu hiyo baada ya makosa ya kipa Ayoub Lakred, Lakini mwamba wa Lusaka Clatous Chama kwa mara nyingi akiirudisha Simba mchezoni dakika ya 93 ya mchezo.

Wekundu wa Msimbazi licha ya kubanwa mbavu ugenini lakini sare inaweza kua ya faida kwao, Kwani wameipata sare hiyo ugenini na mchezo mwingine utapigwa wakiwa nyumbani katika dimba la Chamazi jiji Dar-es-salaam ikiwa ni faida kwa upande wao.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.