Klabu ya Manchester United imeendelea ilipoishia katika mchezo dhidi ya Arsenal wiki mbili zilizopita baada ya leo kupokea kipigo kingine wakiwa katika dimba lao la Old Trafford dhidi ya Brighton.

Manchester United wameendeleza unyonge kwani mpaka sasa msimu huu wameshapoteza michezo mitatu katika michezo mitano ambayo wamecheza mpaka sasa wakiivuka rekodi yao ya msimu ulimalizika.manchester uNITEDMan United leo wamekubali kichapo cha mabao matatu kwa moja kwa mara nyingine kama ambavyo walifungwa  dhidi ya Arsenal, Lakini tofauti leo wamekubali kichapo hicho katika uwanja wao wa nyumbani ambao wamekua hawapotezi mchezo mara kwa mara.

Brighton wameonekana kua wababe wa Man United siku za hivi karibuni kwani katika michezo yao mitatu ya ligi kuu ya Uingereza waliyokutana Brighton wameshinda michezo yote na kufanikiwa kuvunja rekodi ya Man United tena katika dimba lao la Old Trafford.manchester uNITEDManchester United ilikua haijapoteza mchezo wowote wa ligi kuu ya Uingereza tangu walipopoteza dhidi ya Brighton msismu uliomalizika, Brighton ndio wamekuja kuvunja mwiko huo tena leo kwa kuichabanga klabu hiyo kwa mabao matatu kwa moja.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa