Jorrel Hato Atua Chelsea Kwa Mkataba Wa Miaka 7

Kijana mwenye kipaji kikubwa kwenye safu ya ulinzi kutoka Ajax, Jorrel Hato, amekamilisha vipimo vya afya na kusaini mkataba wa miaka saba na Chelsea, huku akiandaliwa kuwa sehemu muhimu ya kikosi cha Enzo Maresca msimu huu mpya.

Jorrel Hato Atua Chelsea, Mkataba Wa Miaka 7 Kwa Kijana Wa Kiholanzi

Beki huyo mwenye umri wa miaka 19 anajiunga rasmi na The Blues baada ya kuonyesha ubora mkubwa akiwa na Ajax, ambapo tayari amecheza zaidi ya mechi 110 katika mashindano yote, rekodi ya kipekee kwa kijana wa umri wake. Msimu uliopita pekee, Hato alicheza mechi 50, 31 kati ya hizo kwenye Eredivisie, akiibeba safu ya ulinzi ya majogoo wa Amsterdam kwa ujasiri mkubwa.

Kwa mujibu wa Fabrizio Romano, Hato anakuwa usajili wa sita wa Chelsea msimu huu wa joto, na anatarajiwa kuungana na kikosi cha Maresca mara moja katika maandalizi ya msimu mpya.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Jorrel Hato Atua Chelsea, Mkataba Wa Miaka 7 Kwa Kijana Wa Kiholanzi

Akiwa ana uwezo mkubwa kucheza kama beki wa kushoto na kati wa ulinzi, Hato analeta ushindani mzuri katika eneo ambalo Chelsea imekuwa na changamoto. Huku Marc Cucurella akiwa ndiye aliyebeba jukumu hilo msimu uliopita kwa kucheza mechi 54, na Ben Chilwell akitarajiwa kuondoka rasmi baada ya muda wake wa mkopo Crystal Palace, nafasi iko wazi kwa kijana huyu kung’ara.

Jorrel Hato Atua Chelsea, Mkataba Wa Miaka 7 Kwa Kijana Wa Kiholanzi

Chelsea wamewekeza kwa muda mrefu kwa kijana huyu, na sasa Stamford Bridge inamkaribisha kwa mikono miwili. Je, Hato ndiye mrithi wa muda mrefu wa beki ya kushoto ya The Blues? Muda utasema lakini dalili zote zinaonyesha nyota mpya inang’aa upande wa magharibi mwa London.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.