Son Heung-Min Kuondoka Tottenham Baada Ya Miaka 10

Nahodha wa Tottenham Hotspur na nahodha wa timu ya taifa ya Korea Kusini, Son Heung-Min, ametangaza rasmi kuwa ataondoka kwenye klabu hiyo majira haya ya joto, na tayari klabu ya Los Angeles FC kutoka MLS inaongoza mbio za kumnasa.

Son Heung-Min Kuondoka Tottenham Baada Ya Miaka 10

Son, ambaye amekuwa nguzo ya Spurs kwa kipindi cha muongo mzima, ametimiza ndoto yake ya kutwaa taji akiwa na Tottenham mwezi Mei, walipoibuka mabingwa wa Europa League kwa ushindi mwembamba wa 1-0 dhidi ya Manchester United, mafanikio yaliyovunja ukame wa miaka 17 bila kombe kwa klabu hiyo ya London Kaskazini.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari nchini Korea Kusini, kabla ya mechi ya kirafiki dhidi ya Newcastle siku ya Jumapili, Son alifichua kuwa huu ni wakati sahihi wa kutafuta changamoto mpya.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

“Kabla hatujaanza, ningependa kusema kuwa nimeamua kuondoka klabuni majira haya ya joto,” alisema Son mbele ya waandishi.

“Kwa heshima kubwa, klabu inanisaidia katika kufanikisha maamuzi haya. Hili ni moja ya maamuzi magumu zaidi niliyowahi kufanya katika maisha yangu ya soka.”

Son Heung-Min Kuondoka Tottenham Baada Ya Miaka 10

Baada ya kuvaa jezi ya Spurs mara 454 na kufunga mabao 173, Son anasema ni muda wa kuhamia mazingira mapya.

“Nahitaji mazingira mapya ya kunisukuma zaidi. Mabadiliko kidogo ni muhimu, miaka 10 ni muda mrefu sana,” alisema kwa hisia.

“Nilikuja London Kaskazini nikiwa na umri wa miaka 23, kijana mdogo sana. Leo naondoka nikiwa mtu mzima, mwenye fahari kubwa.”

Son hakusahau kuwatumia ujumbe mashabiki wa Tottenham:

“Nawashukuru mashabiki wote wa Spurs kwa upendo wao wa kipekee. Naamini huu ndio wakati muafaka wa kusema kwaheri, na natumai kila mmoja ataelewa na kuheshimu uamuzi wangu.”

Son Heung-Min Kuondoka Tottenham Baada Ya Miaka 10

Alijiunga na Spurs mwaka 2015 akitokea Bayer Leverkusen na licha ya msimu wa kwanza kuwa mgumu, aligeuka kuwa kipenzi cha mashabiki, mchezaji wa kiwango cha juu kwenye EPL, na hata kuibuka mfungaji bora wa ligi msimu wa 2022/23.

Sasa, nyota huyo anajiandaa kufungua ukurasa mpya, lakini historia yake ndani ya Tottenham itasalia kama hadithi ya kishujaa ya mchezaji aliyetoka kuwa kijana hadi kuwa gwiji halisi.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.