England imekumbana na kipigo kikubwa cha mabao 3-1 dhidi ya Senegal katika mechi iliyopigwa kwenye uwanja wa Nottingham Forest, ikiwa ni mara ya kwanza kwa Thomas Tuchel kutokupata ushindi kama kocha wa Simba Watatu.

Mechi ilianza na kasi kwa Waingereza hao, na kumpelekea Harry Kane kufunga bao la kwanza la mapema kabisa dakika ya saba baada ya Anthony Gordon kupiga mpira wa chini uliozuiwa na kipa Edouard Mendy kisha kumkuta Kane aliyeupiga golini. Hata hivyo, walipoteza nafasi ya kuongoza 2-0 dakika ya 28 baada ya Gordon kushindwa kuitumia vizuri krosi iliyopigwa na Kyle Walker.
Senegal, waliokuwa wakizidi kupata nguvu kadri mechi ilivyosonga, walipata bao la kusawazisha kabla ya mapumziko ya nusu ya mchezo kupitia Ismaila Sarr, ambaye alifaidika na pasi ya Nicolas Jackson baada ya mpira wa juu kuipita safu ya ulinzi ya England huku Walker akijaribu kuuokoa lakini akishindwa kuufikia mpira huo.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Mpaka mapumziko, ubao ulikuwa ukisoma 1-1 lakini vijana hao wa Tuchel walishindwa kurekebisha makosa ya awali, kwani mpira mwingine wa juu uliwapa Senegal bao la pili kupitia Habib Diarra, ambaye alimpita Myles Lewis-Skelly na kumfunga Henderson. England walipata nafasi za kurejesha mzani sawa kupitia kwa Gibbs-White pamoja na Saka, lakini Mendy alikuwa imara langoni.

Jude Bellingham alifanikiwa kufunga bao lakini lilikataliwa na VAR kwani mpira huo ulichezwa kwa mkono kwa Levi Colwill. Senegal walimalizia mechi kwa bao la tatu la Cheikh Sabaly, na kuifanya iwe siku ngumu na ya kusikitisha kwa England.

