Memphis Depay alifanikiwa kufunga mabao mawili kwenye ushindi wa mabao 8-0 dhidi ya Malta jumanne kwenye mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia na kufikisha rekodi ya magoli 50 ya timu ya taifa ya Uholanzi, sawa na rekodi ya Robin van Persie.

Memphis Depay alifunga bao la kwanza dakika ya tisa kwa penati na kuongeza la pili dakika saba baadaye kwa shuti la nguvu, na kufanikiwa kufikisha idadi ya magoli 50 katika mechi 102 akiichezea Uholanzi.
Mchezaji wa pembeni Donyell Malen, ambaye aliingia kuchukua nafasi ya Memphis Depay, naye alifunga mabao mawili, huku nahodha Virgil van Dijk, Xavi Simons, Noa Lang, na Micky van de Ven wakiongeza bao mojamoja, na kuwapa Uholanzi ushindi wa pili mfululizo katika Kundi G baada ya kuwashinda Finland huko Helsinki Jumamosi.

Bila kusahauΒ meridianbetΒ ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Bao la kwanza la Depay katika uwanja wa Euroborg lilikuja baada ya Justin Kluivert kufanyiwa madhambi ndani ya eneo la penati. Bao la pili lilikuwa mpira uliorudishwa kutoka mstari wa pembeni na Depay akaupiga kwa nguvu kutoka pembezoni mwa eneo la penati. Van Dijk alifunga bao la 3 baada ya dakika 20 kwa shuti, huku Simons akifunga bao la nne dakika ya 61 baada ya Uholanzi kuwa wamepoteza nafasi nyingi.

Timu hiyo ilifidia nafasi zilizopotea kwa kufunga mabao manne katika dakika 16 za mwisho, huku Malen akiutawala mchezo. Mshambuliaji huyo wa Aston Villa alifunga bao la tano baada ya Van de Ven kurudisha mpira nyuma dakika ya 74, kabla ya pasi iliyopigwa vizuri kwa Lang kufunga bao la sita dakika nne baadaye. Malen aliongeza bao lake la pili dakika ya 80, na Van de Ven, ambaye alikuwa akicheza kutokea upande wa kushoto kwa muda mwingi, akafunga bao dakika za lala salama.

Kocha wa Uholanzi Ronald Koeman aliwaacha nje baadhi ya wachezaji wake walipata kadi za njano katika mechi dhidi ya Finland ili kuepuka kusimamishwa kwa wachezaji katika mechi yao ya nyumbani dhidi ya Poland mwezi Septemba, ambayo inaweza kuwa mechi ya maana katika kundi hili.


