Timu ya taifa ya Uholanzi imefanikiwa kuanza michuano ya Euro mwaka 2024 kwa matokeo ya ushindi baada ya kuifunga timu ya taifa ya Poland kwa jumla ya mabao mawili kwa moja.
Uholanzi ambao walianza kutanguliwa katika mchezo huo baada ya timu ya taifa ya Poland kupata bao la mapema dakika ya 16 kupitia kwa mshambuliaji wao Adam Buksa, Lakini kabla ya mapumziko vijana wa kocha Ronald Koeman walisawazisha bao dakika ya 29 kupitia kwa Coady Gapko na matokeo kwenda mapumziko kwa sare ya bao moja kwa moja.Mchezo huu ulionekana kua na kasi na timu zote zikiwa zinashambulia kwa zamu ikiwa ni wazi kila timu ikionekana inahitaji matokeo ya ushindi, Kipindi cha pili kiliendelea kwa kasi kama ambavyo kipindi cha kwanza ambapo kipindi cha pili mwanzoni Poland wakionekana kuhitaji goli la uongozi kwa kiwnago kikubwa.