Aston Villa Kuipiku Arsenal kwa Onana

Klabu ya Aston Villa inaweza kuipiku klabu ya Arsenal katika kuwania saini ya kiungo wa kimataifa wa Ubelgiji anayekipiga klabu ya Everton Amadou Onana ambaye alikua anafuatiliwa kwa karibu na klabu ya Arsenal.

Aston Villa wanaelezwa kuanza kumtolea macho kiungo Amadou Onana ambaye kw amuda mrefu sasa klabu ya Arsenal imekua na mpango haswa katika dirisha hili kubwa baada ya kutokumsajili kwenye dirisha dogo la Janauari, Hivo klabu hiyo yenye maskani yake Villa Park imekua mstari wa mbele sasa kumtaka kiungo huyo.

Sababu ya klabu hiyo kua mstari wa mbele kumtaka Amadou Onana ni kuondoka kwa kiungo wake raia wa kimataifa wa Brazil Douglas Luiz ambaye yupo mbioni kujiunga na klabu ya Juventus ya nchini Italia, Hivo kumpata Amadou Onana kwao wanaona ni mbadala sahihi sana kwa kiungo wao wa kimataifa wa Brazil.aston villaArsenal wamekua wakimfukuzia Amadou Onana kwa miezi sasa lakini hawakufanikiwa kupeleka ofa rasmi kwa klabu ya Everton, Huku taarifa zinaeleza kua Aston Villa hawataki kupoteza muda wanajiandaa kupeleka ofa kwa klabu ya Everton mapema ili kuweza kukamilisha dili hilo mapema.

Acha ujumbe