Uingereza Kutupa Karata yake ya Kwanza Euro2024 Leo

Timu ya taifa ya Uingereza leo inatupa karata yake ya kwanza kwenye michuano ya Euro 2024 ambayo imeanza Ijumaa ya tarehe 14 mwezi huu wenyeji Ujerumani wakifungua dhidi ya Scotland.

Uingereza ikiwa ni moja ya timu zinazosubiriwa zaidi kwenye michuano hiyo leo watashuka dimbani kukipiga dhidi ya taifa ya Serbia kwenye mchezo wao wa kwanza wa kundi C, Mchezo ambao unatarajiwa kua wenye ushindani mkubwa kwakua timu ya taifa ya Serbia pia wana timu ya ushindani.UingerezaKinachofanya Uingereza isubiriwe kwa hamu zaidi kwenye michuano hiyo ni kutokana  na ubora wao, majina ambayo wanayo kwenye kikosi chao, lakini pia ni moja ya timu ambazo zinapewa nafasi ya kutwaa taji la michuano hiyo baada ya kucheza vizuri kwenye michuano iliyopita na kufankiwa kucheza fainali.

Siku za hivi karibuni timu hiyo imekua ikifanya vizuri kwenye michuano ambayo wamekua wakishiriki na wamefanikiwa kutengeneza kizazi bora sana ambacho kimekua na wachezaji bora sana kwenye maeneo mbalimbali uwanjani, Kitu ambacho timu hiyo inakosa mpaka sasa ni kutwaa taji tu.UingerezaBaada ya kucheza fainali ya michuano ya Euro 2020 dhidi ya timu ya taifa ya Italia na kufungwa kwenye changamoto ya mikwaju ya penati, Leo Uingereza wanaanza safari ya kuhakikisha wanalitwaa taji hilo mbele ya timu ya taifa ya Serbia wakiwa ni moja timu yenye vipaji vya hali ya juu kwenye michuano hiyo.

Acha ujumbe