Karia Awaonya Waamuzi Kuelekea Msimu Mpya

Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia, ametoa onyo kali kwa waamuzi wote watakaoshiriki katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu ujao, akieleza wazi kwamba hakuna utaratibu wa kuvumilia makosa makubwa. Aliyasema hayo wakati wa kuitimisha Semina maalumu ya waamuzi iliyofanyikia makao makuu ya TFF, Ilala Dar es Salaam.

“Huu ni msimu tunaotarajia utakuwa tofauti sana, tukimaliza tutapongezana, lakini kwa wale watakaokuwa tofauti tutakuwa tumeachana nao moja kwa moja,” amesema Karia. Aliongeza kuwa hali hii si ya utani na kwamba TFF tayari ina mpango wa kuhakikisha waamuzi wanafuata taratibu za usahihi katika michezo yote ya ligi.

Karia Awaonya Waamuzi Kuelekea Msimu Mpya

Karia amesema kuwa TFF ipo na utaratibu maalumu kupitia kamati ya waamuzi na paneli ya kujadili utendaji wa waamuzi. “Mwenyekiti wa Kamati ya Usimamizi wa Ligi, kama utaendelea na utaratibu wa kuangalia matukio ya ligi, naomba sana waamuzi ambao mtawaona wana hitilafu, nyie warudisheni katika paneli. Paneli hiyo itafanya kazi yake ikishirikiana na vyombo vingine,” amesema.

Aidha, Karia alikumbusha matukio ya msimu uliopita ambapo makosa ya waamuzi yalisababisha mtikisiko mkubwa nchini hadi kufikia serikali kuingilia kati. Alisisitiza kuwa Tanzania imeshafikisha mpira wake sehemu kubwa ambapo dunia nzima inatambua maendeleo ya ligi, na kwamba ni lazima waamuzi wasiwe chanzo cha kuporomoka kwa soka la nchi.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Karia Awaonya Waamuzi Kuelekea Msimu Mpya

“Huu mpira wetu tumeshaufikisha sehemu kubwa sana ambayo Dunia nzima inatutambua sasa, hivyo tusiwe chanzo cha kuporomoka,” Karia ameongeza.

Onyo hili la TFF linakuja wakati ligi inajiandaa kuanza msimu mpya, na linatuma ishara dhahiri kuwa utendaji wa waamuzi ni kipengele muhimu kinacholindwa kwa nguvu ili kuhakikisha ushindani wa haki na waadilifu kwenye dimba.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.