Vardy Afungua Ukurasa Mpya Italia

Mshambuliaji wa zamani wa Leicester City, Jamie Vardy, ameanza rasmi sura mpya ya maisha yake ya soka kwa kujiunga na klabu ya Serie A ya Cremonese, akisisitiza kuwa “umri ni nambari tu” huku akiwa na miaka 38.

Vardy, ambaye anahesabiwa miongoni mwa wachezaji bora kabisa kuwahi kuichezea Leicester, alihitimisha safari yake ya miaka 13 na klabu hiyo mwishoni mwa msimu uliopita. Katika kipindi hicho, alifunga mabao 200 katika mechi 500, ikiwemo mabao 24 aliyofunga msimu wa 2015-16 walipotwaa ubingwa wa Premier League.

Jamie Vardy Afungua Ukurasa Mpya Italia

Mapema mwezi huu, Vardy alisaini mkataba wa uhamisho huru na Cremonese, timu iliyopanda daraja msimu huu, na huenda akacheza mechi yake ya kwanza Jumatatu dhidi ya Verona. Akizungumza kuhusu motisha ya wachezaji wakongwe kama Kevin De Bruyne na Luka Modrić waliotua Serie A msimu huu, Vardy alijibu kwa ujasiri;

“Kwangu mimi, umri si kikwazo. Mradi miguu yangu bado inafanya kazi kama zamani na ninajihisi mchangamfu, nitaendelea kucheza. Kwa sasa hakuna dalili za kupungua kasi, kwa hiyo nitaendelea kupambana na kutoa kila kitu kwa klabu hii.”

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Cremonese wameanza msimu kwa kishindo, wakishinda mechi yao ya ufunguzi kwa mabao 2-1 dhidi ya AC Milan, kabla ya kuichapa Sassuolo 3-2. Matokeo haya yamewapa matumaini makubwa ya kufanya vizuri ligi kuu msimu huu.

Jamie Vardy Afungua Ukurasa Mpya Italia

Akikumbuka enzi zake Leicester, Vardy alifafanua kuwa lengo kuu si kutwaa mataji bali kuhakikisha timu inabaki kwenye ligi;

“Hata kule Leicester haikuwa kuhusu ‘tunaenda kutwaa hili’, bali ‘tunapaswa kusalia kwenye ligi’. Hilo ndilo jambo la msingi. Kwa hiyo, unachofanya ni kuchukulia kila mechi kama fursa mpya, unajituma, na matokeo yatakuja yenyewe.”

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.