Simba Wameanza Kuwapigia Hesabu  Al Ahly

Klabu ya Simba ni kama tayari imejithibitishia kuwa itakwenda kucheza hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika na tayari wameanza kuota ni mpinzani gani wanataka kucheza naye, baada ya Afisa habari wake Ahmed Ally kusema kuwa, wanatamani kupangwa kundi moja na Al Ahly. 

Ahmed, amesema kikosi hicho kimeweka dhamira kubwa kuelekea mechi ya marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Nsingizini Hotspurs ya Eswatini, akisisitiza kuwa hii ni mechi ya kihistoria kwa klabu hiyo na haipaswi kuchukuliwa kwa urahisi.

Simba Wameanza Kuwapigia Hesabu  Al Ahly

Na wakipenya hapo watakuwa na kikasi na timu zote kubwa  za Afrika kama Al Ahly ambao waliwahi kukatisha safari yao ya kwenda nusu fainali ya mashindano hayo misimu kadhaa nyuma.

Simba inatarajia kushuka dimbani Oktoba 26, 2025 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam, ikiwa na kumbukumbu ya ushindi wa mabao 3–0 ilioupata kwenye mechi ya kwanza ugenini.

“Kwetu huu ni mchezo muhimu kwelikweli. Ni mchezo unaoenda kuandika historia ya kupendeza. Tunaenda kujiweka katika kundi la klabu kubwa barani Afrika vyenye uhakika wa kucheza hatua ya makundi kila mwaka.

“Na tunatamani tukutane na wakubwa wenzetu wa Afrika kama Al Ahly ili tuendelee kuonesha umwamba kwenye mashindano haya na hiyo ndiyo dhamira yetu na itakwenda kutimia,” amesema.

 Amefafanua kuwa, Simba ipo katika njia ya kujiunga na klabu mbili pekee zilizoonyesha ubora katika michuano ya CAF ndani ya miaka saba iliyopita, akizitaja kuwa ni Al Ahly ya Misri na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini.

Simba Wameanza Kuwapigia Hesabu  Al Ahly

 “Katika kipindi cha miaka saba, timu ambazo zimekuwa na uhakika wa kucheza makundi ni Al Ahly na Mamelodi. Lakini sasa wa tatu anaenda kuongezeka na huyo ni Simba. Hiyo ni heshima kubwa sana kwetu.”

 Ahmed amesema mechi hiyo sio ya kawaida kwa sababu inawakilisha hadhi na heshima ya klabu ndani ya bara la Afrika, hivyo kila shabiki anatakiwa kulitambua hilo.

“Mwanasimba hatakiwi kwa namna yoyote kubaki nyumbani. Hatutaki mtu aseme ‘tumeshinda ugenini, tumemaliza kazi.’ Hapana! Hii mechi ni kama hatujacheza bado,” amesema.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa.

Simba Wameanza Kuwapigia Hesabu  Al Ahly

 Rekodi zinaonyesha katika miaka saba ambayo Ahmed Ally ameizungumzia, Simba imecheza hatua ya makundi ya michuano ya CAF mara tano ambayo ni msimu wa 2020–2021 (Ligi ya Mabingwa), 2021–2022 (Kombe la Shirikisho), 2022–2023 (Ligi ya Mabingwa), 2023–24 (Ligi ya Mabingwa) na 2024-2025 (Kombe la Shirikisho). Ikifuzu safari hii itakuwa ya sita mfululizo inakwenda kucheza makundi.

Katika mara zote hizo ilizofuzu makundi, pia imefanikiwa kwenda hadi robo fainali na kuishia hapo, lakini msimu uliopita 2024-2025 ilicheza fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika ikipoteza mbele ya RS Berkane. Kabla ya hapo, Simba pia ilicheza robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu wa 2018–2019.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.