Phillips Apata Njia ya Kutoroka Manchester City

Kalvin Phillips, aliyewahi kuwa nguzo ya kikosi cha England, sasa anaweza kupata mlango wa kutokea Manchester City baada ya Wolverhampton Wanderers kuonyesha nia ya kumsajili katika dirisha la usajili la Januari. Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 30 amekuwa kivuli Etihad, akicheza mechi moja tu msimu huu chini ya Pep Guardiola.

Kwa mujibu wa Daily Mail, Wolves waliopo mkiani mwa msimamo wa ligi wameanza kufanya hesabu za mwisho kabla ya dirisha la usajili kufungwa Februari 2. Klabu hiyo ya Molineux inaaminika kuwa mashabiki wa muda mrefu wa Phillips na inaangalia uwezekano wa kumsajili, hasa ikizingatiwa kuwa Joao Gomes na Andre wanawaniwa na vilabu vingine.

Phillips Apata Njia ya Kutoroka Manchester City

Timu ya Rob Edwards imekuwa katika hali nzuri siku za karibuni, ikicheza michezo mitano mfululizo bila kupoteza katika Ligi Kuu na FA Cup. Wolves wanaamini uzoefu wa Phillips unaweza kuwa silaha muhimu katika mapambano ya kujiokoa dhidi ya kushuka daraja, hasa kipindi hiki ambacho ushindani unazidi kuwa mkali.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Phillips alijiunga na Manchester City mwaka 2022 akitokea Leeds United kwa ada ya pauni milioni 42, lakini hakuwahi kupata nafasi ya kudumu. Baada ya kuonekana mara 21 msimu wake wa kwanza, alicheza mechi 10 tu msimu uliofuata kabla ya kutupwa kwa mkopo West Ham na baadaye Ipswich Town, ambako alishuhudia timu hiyo ikishuka daraja. Msimu huu, mchango wake pekee ulikuwa kuingia kama mchezaji wa akiba dhidi ya Huddersfield Town kwenye Carabao Cup.

Phillips Apata Njia ya Kutoroka Manchester City

Safari ya Phillips City pia imegubikwa na kumbukumbu nzito ya kauli ya Guardiola aliyomuita mzito kupita kiasi baada ya Kombe la Dunia 2022. Ingawa kocha huyo aliomba radhi miaka miwili baadaye, Phillips alikiri kauli hiyo ilimuumiza. Sasa, Wolves wanaweza kuwa nafasi ya mwisho kwa kiungo huyo kuokoa heshima yake, kurejesha makali yake, na kuthibitisha kuwa bado ana nafasi katika soka la juu.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.