Arteta Ajibu Lawama Za Kupoteza Muda kwa Kona

Kocha wa Arsenal FC, Mikel Arteta, Jumanne alipuuza vikali lawama zinazoelekezwa kwa timu yake kuhusu mbinu za mipira ya adhabu ya kona, akikanusha madai ya kupoteza muda na kueleza kusikitishwa kwake na ukweli kwamba kikosi chake hakifungi mabao mengi zaidi kupitia kona.

Arteta Ajibu Lawama Za Kupoteza Muda kwa Kona, Asema Arsenal Wanataka kuwa Bora Kila Idara

Arsenal, vinara wa Premier League, tayari wamefunga mabao 16 yatokanayo na kona msimu huu, wakifikia rekodi ya ligi hiyo huku zikiwa zimesalia mechi tisa kabla ya msimu kumalizika. Hata hivyo, mafanikio hayo yamezua mjadala kuhusu mabadiliko ya kiufundi katika matumizi ya mipira ya adhabu, huku baadhi ya wapinzani wakieleza kutoridhishwa na utaratibu wa Arsenal wanapopiga kona.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Lawama hizo ziliongezwa na kocha wa Brighton & Hove Albion, Fabian Hurzeler, ambaye alidai kuwa wakati mwingine Arsenal hutumia zaidi ya dakika moja kupiga kona. Hata hivyo, Arteta hakuonesha kujali malalamiko hayo akisema ni sehemu ya kazi katika soka la kisasa.

Arteta Ajibu Lawama Za Kupoteza Muda kwa Kona, Asema Arsenal Wanataka kuwa Bora Kila Idara

Arteta alieleza kuwa mabadiliko ya kimkakati katika soka yamesababisha timu nyingi kupunguza nafasi za mashambulizi ya wazi, hali inayolazimisha ubunifu zaidi katika mipira ya adhabu. Alisisitiza kuwa timu sasa zinajiandaa kwa kila tukio uwanjani, iwe ni mpira wa kurushwa, kuanzisha upya mchezo au mashambulizi ya wazi, na mara nyingi ulinzi huwa wa mtu kwa mtu.

Arteta Ajibu Lawama Za Kupoteza Muda kwa Kona, Asema Arsenal Wanataka kuwa Bora Kila Idara

 

Kwa upande wake, Hurzeler alitaka kuwepo kwa kanuni zilizo wazi zaidi kuhusu usimamizi wa muda wa mchezo, akisema mashabiki wanaolipia viingilio vya gharama kubwa wanastahili kuona muda halisi wa mchezo ukiwa sawa katika kila mechi. Alibainisha kuwa mara nyingi muda halisi wa mpira kuwa uwanjani huwa takribani dakika 50 badala ya 65.

Arteta Ajibu Lawama Za Kupoteza Muda kwa Kona, Asema Arsenal Wanataka kuwa Bora Kila Idara

Kwa sasa Arsenal wanaongoza msimamo wa Premier League kwa tofauti ya pointi tano dhidi ya mabingwa watetezi Manchester City, ingawa wamecheza mechi moja zaidi ya wapinzani wao hao.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.