Wakala wa Haaland Akanusha Mazungumzo na Barcelona

Rafaela Pimenta wakala wa mshambuliaji wa Manchester City, Erling Haaland, amekanusha taarifa zinazoeleza kuwa kuna mazungumzo ya kumpeleka nyota huyo katika klabu ya FC Barcelona.

Wakala wa Haaland Akanusha Mazungumzo na Barcelona

Taarifa hizo ziliibuka Alhamisi zikidai kuwa mmoja wa wagombea wa urais wa Barcelona, Víctor Font, alikuwa akifanya mazungumzo ya kuhakikisha klabu hiyo inapata nafasi ya kwanza ya kumsajili Haaland endapo atachaguliwa kuwa rais wa klabu hiyo. Hatua hiyo ilitajwa kuwa ingeweza kuwa silaha kubwa ya kisiasa katika uchaguzi wa Barcelona ili kumpa ushindani mkali rais wa sasa Joan Laporta ambaye anaonekana kuwa na nafasi kubwa ya kuchaguliwa tena.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Wakala wa Haaland Akanusha Mazungumzo na Barcelona

Hata hivyo, wakala wa Haaland, Rafaela Pimenta, amekanusha vikali taarifa hizo akisisitiza kuwa hakuna mawasiliano yoyote yaliyofanyika kati ya Barcelona na mchezaji huyo au uongozi wake.

Akizungumza katika mahojiano maalum na kituo cha michezo El Chiringuito, Pimenta amesema wana heshima kubwa kwa Barcelona lakini hawajawahi kuwasiliana nao kuhusu suala la uhamisho wa Haaland.

Wakala wa Haaland Akanusha Mazungumzo na Barcelona

Aidha aliongeza kuwa Haaland aliongeza mkataba wake na Manchester City miezi michache iliyopita na ana furaha kubwa kuendelea kucheza katika klabu hiyo, hivyo kwa sasa hakuna mazungumzo yoyote kuhusu uhamisho wake kwani mambo yanaenda vizuri katika timu hiyo.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.