Penalti ya Taborda Yaipa Panathinaikos Ushindi Dhidi ya Real Betis

Panathinaikos FC imepata ushindi muhimu wa bao 1-0 dhidi ya Real Betis katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa hatua ya 16 bora ya UEFA Europa League baada ya yakupata mkwaju wa penalti ya dakika za mwisho na kufungwa na Vicente Taborda.

Penalti ya Taborda Yaipa Panathinaikos Ushindi Dhidi ya Real Betis

Mchezo ulianza kwa tahadhari kutoka kwa timu zote mbili huku nafasi za kufunga zikiwa chache. Nafasi bora ya awali ilitokea pale Cucho Hernández alipiga kichwa kilichookolewa kwa ustadi na kipa Alban Lafont.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Kadri mchezo ulivyoendelea, Betis walionekana kutawala zaidi kwa kumiliki mpira kwa zaidi ya asilimia 70 huku wakilazimisha mipira kadhaa ya kona. Hata hivyo, Panathinaikos walipata nafasi yao ya kwanza dakika ya 15 lakini Georgios Kyriakopoulos alikosa shabaha kwa kupiga shuti lililotoka nje mbali na lango.

Penalti ya Taborda Yaipa Panathinaikos Ushindi Dhidi ya Real Betis

Dakika chache kabla ya mapumziko, Hernández alikaribia kufunga kwa shuti la chini lililolazimisha Lafont kufanya kazi ya ziada kuokoa, lakini pamoja na Betis kutawala mchezo katika kipindi cha kwanza hawakuweza kubadili umiliki huo kuwa mabao.

Kipindi cha pili kilianza kwa Panathinaikos kuonyesha dalili za kushambulia zaidi kupitia Facundo Pellistri huku Andrew Tetteh akidai penalti ambayo haikutolewa. Hata hivyo, mambo yalibadilika pale Anass Zaroury alipopewa kadi ya pili ya njano na kutolewa nje, na kuiacha Panathinaikos wakicheza na wachezaji 10.

Penalti ya Taborda Yaipa Panathinaikos Ushindi Dhidi ya Real Betis

Licha ya kucheza pungufu, Panathinaikos walipata nafasi ya kuamua mchezo dakika za mwisho baada ya Karol Świderski kuangushwa na Diego Llorente ndani ya eneo la hatari. Baada ya mapitio ya VAR, penalti ilitolewa na Llorente akaonyeshwa kadi nyekundu.

Hatimaye Taborda alifunga penalti hiyo dakika ya 87 na kuipatia Panathinaikos ushindi muhimu katika Uwanja wa Apostolos Nikolaidis Stadium. Ushindi huo unaendeleza rekodi nzuri ya timu hiyo nyumbani ambapo imepoteza mchezo mmoja tu kati ya 13 iliyocheza hivi karibuni katika uwanja huo.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.