Afisa habari wa Yanga SC, Ally Shaaban Kamwe, amesema kuwa timu yake itacheza mchezo dhidi ya TRA FC katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha huku masaa 72 ya kupumzika kati ya michezo hayajatimia.
Akizungumza na waandishi wa habari, Kamwe alisisitiza kuwa suala hilo ni muhimu sana na limekuja kama changamoto kubwa kwa wachezaji kucheza mechi bila kupata muda wa kutosha wa kupumzika.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Aidha, Kamwe aliongeza kuwa hoja kuhusu penati katika mechi dhidi haikufuata kwa uangalifu, na badala yake, waandishi walifuata watu ambao hawahusiki na mechi hiyo.
“Sisi Yanga tumemuachia mungu suala hilo, kwani kila mtu ameona kilichotokea, lakini watu hawaulizii chochote,” alisema Kamwe.
Tukio hili linaongeza mjadala kuhusu haki na usawa wa kucheza katika mashindano ya Ligi Kuu ya NBC, huku mashabiki wakitarajia mechi hiyo itakayopigwa kwa kiwango cha juu licha ya changamoto ya kupumzika kwa wachezaji.

