Kocha wa Pep Guardiola ameweka wazi kuwa kikosi cha sasa cha Manchester City bado hakijafikia ubora wa miaka ya nyuma, kufuatia kuondolewa kwenye UEFA Champions League na Real Madrid kwa msimu wa tatu mfululizo.
City walipoteza kwa mabao 2-1 katika mchezo wa marudiano uliochezwa Uwanja wa Etihad, huku Vinícius Júnior akifunga mabao mawili yaliyowapa ushindi Madrid. Nahodha Bernardo Silva alitolewa kwa kadi nyekundu mapema dakika ya 20 baada ya kuokoa mpira kwa mkono kwenye mstari wa goli.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Matokeo hayo yaliongeza machungu baada ya kipigo kizito cha awali kilichochezwa Uwanja wa Santiago Bernabéu, ambapo Federico Valverde alifunga hat-trick na kuipa Madrid faida kubwa ya jumla ya mabao 6-3 dhidi ya City.
Licha ya kuondolewa, Guardiola anaamini timu yake ipo kwenye hatua ya kujijenga upya baada ya kufanya mabadiliko makubwa ya kikosi katika vipindi vitatu vya usajili vilivyopita, huku akisisitiza kuwa muda unahitajika kurejesha uimara wa zamani.
“Bado hatujakamilika. Kuna mambo katika nyakati fulani tunahitaji kuwa makini zaidi, lakini naamini ni suala la muda,” alisema Guardiola.
“Tumewahi kuwa timu kamili katika kila idara, lakini sasa bado hatujafikia kiwango hicho. Tunahitaji kumaliza ligi vizuri, kufanya maamuzi sahihi wakati wa majira ya usajili, na msimu ujao tutarejea tena kwenye Ligi ya Mabingwa,”

