Morocco Yazindua Jezi Maalum Za Ubingwa Kufuatia Ushindi wa AFCON 2025

Baada ya kutawazwa rasmi kuwa Mabingwa wa AFCON 2025, Morocco Simba wa Atlas wameamua kusherehekea kwa staili ya kipekee. timu ya taifa imezindua jezi maalum za ubingwa, zinazotambulisha mafanikio yao ya kihistoria ya ubingwa wa ‘mezani’.

Morocco Yazindua Jezi Maalum Za Ubingwa Kufuatia Ushindi wa AFCON 2025Jezi hii mpya inajivunia nyota ya pili kifuani, ikiwakilisha ushindi wao wa pili wa AFCON baada ya miaka mingi ya kusubiri. Kwa mara ya kwanza, nyota hii inakiri historia na mafanikio mapya ya timu ya taifa.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa  

Ubunifu wa kitamaduni umejumuishwa kwenye jezi kwa kutumia nakshi za ‘Zellij’ sanaa ya vigae vya kimoroko vilivyochorwa kwa ustadi kwenye mabega na upande wa ubavu, ikionyesha utambulisho wa taifa na urithi wa kiutamaduni.

Morocco Yazindua Jezi Maalum Za Ubingwa Kufuatia Ushindi wa AFCON 2025Aidha, nembo ya CAF pamoja na namba za wachezaji zimepambwa kwa rangi ya dhahabu inayong’ara, ikionyesha utukufu wa ubingwa huu na kuimarisha heshima ya Morocco barani Afrika.

Jezi hizi za kipekee sasa zinatumika kusherehekea ushindi wa Morocco, huku zikionyesha fahari, historia, na utamaduni wa taifa lililoongoza kwenye soka la Afrika.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.