Ryan Giggs Anaunga Mkono Man United Kumrudisha Højlund Ili Apambane na Benjamin Sesko.

Ryan Giggs ambaye ni nguli wa  Manchester United anaunga mkono klabu hiyo kumrudisha Højlund ili aweze “kupambania nafasi” kikosini pamoja na Benjamin Sesko.

Ryan Giggs Anaunga Mkono Man United Kumrudisha Højlund Ili Apambane na Benjamin Sesko.

United wameendelea kuimarika chini ya Michael Carrick, huku nafasi ya kushiriki UEFA Champions League msimu ujao ikiwa karibu kuthibitishwa. Pia kunatarajiwa kuwa na usajili mkubwa ili kuifanya timu iweze kushindana barani Ulaya.

Hata hivyo, bado kuna maamuzi muhimu kuhusu baadhi ya wachezaji waliopo nje ya klabu kwa mkopo. Marcus Rashford, Jadon Sancho na Højlund kwa sasa wote wanacheza kwa mkopo barani Ulaya.

Barcelona wana chaguo la kumnunua Rashford, wakati mkataba wa Sancho Old Trafford unaelekea kumalizika msimu huu wa joto. Kwa upande wa Højlund, Napoli wana wajibu wa kumnunua iwapo watafanikiwa kufuzu Champions League hali ambayo inaonekana kuwa karibu kwani wako nafasi ya tatu na wanaongoza kwa pointi nane dhidi ya nafasi ya tano.

Hata hivyo, kati ya wachezaji hao watatu, Højlund ndiye ambaye Giggs angependa kuona akirejea United.

Akizungumza kwenye kipindi cha Rio Ferdinand Presents, Giggs alisema Carrick ana maamuzi makubwa ya kufanya kuhusu wachezaji kama Rashford, Højlund na Sancho. Aliongeza kuwa Højlund hakupata bahati kwani alikuwa mshambuliaji pekee wa kati klabuni, huku matarajio makubwa yakiwekwa juu yake tangu alipowasili.

Ryan Giggs Anaunga Mkono Man United Kumrudisha Højlund Ili Apambane na Benjamin Sesko.

Giggs alieleza kuwa anaamini Šeško anaweza kupata nafasi nyingi zaidi na kufunga mabao zaidi, lakini akasisitiza kuwa kuwa na washambuliaji wawili vijana na wenye njaa ya mafanikio kunaweza kuleta ushindani mzuri kikosini.

Aliongeza kuwa ushindani huo ni moja ya nguvu za Manchester United kwa muda mrefu, ambapo hata mazoezini kunakuwa na ushindani mkubwa, hasa ukiwa na mabeki wa kati wenye ubora wakijaribu kuwazuia washambuliaji kama Šeško.

Kwa upande mwingine, Giggs pia angependa kuona Carrick akiendelea kuwa kocha wa kudumu wa Manchester United. Carrick aliteuliwa kama kocha wa muda hadi mwisho wa msimu, lakini kutokana na kazi nzuri anayofanya, wengi wanaamini anastahili kupewa nafasi ya kudumu  akiwemo Giggs mwenyewe.

Giggs alisema Carrick ameonyesha uongozi thabiti na mtindo wa utulivu katika kuendesha timu. Alivutiwa na namna United walivyocheza dhidi ya Manchester City, wakionesha mtindo wa “pasi na sogea” ambao ni sehemu ya utamaduni wa klabu hiyo.

Ryan Giggs Anaunga Mkono Man United Kumrudisha Højlund Ili Apambane na Benjamin Sesko.

Aliongeza kuwa Manchester United siku zote imekuwa ikipewa sifa kwa kucheza soka la kasi ya mpira kuliko mchezaji, jambo lililoonekana katika michezo ya hivi karibuni.

Giggs alihitimisha kwa kusema angependa kuona Carrick anapata maandalizi kamili ya kabla ya msimu (pre-season) pamoja na nafasi ya kusajili wachezaji anaowahitaji ili kuijenga timu zaidi.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.