Klabu ya Bayern Munich imefanikiwa kutinga fainali ya DFB-Pokal baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Bayer Leverkusen, katika mchezo wa nusu fainali uliowapa nafasi ya kuendelea kusaka mataji msimu huu.
Mchezo ulianza kwa kasi kubwa ambapo Bayern walikaribia kufunga mapema kupitia Luis Díaz, lakini shuti lake lilikataliwa na kipa Mark Flekken, kabla ya shambulizi kali la Bayern kuzaa bao la kwanza kupitia Harry Kane baada ya pasi ya Jamal Musiala.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Kane alisema baada ya mchezo “Ni muhimu sana kwa timu kufika fainali. Tunataka mataji yote msimu huu na kila mchezo ni hatua muhimu kuelekea lengo hilo.”
Bayern waliendelea kutawala mchezo kupitia Joshua Kimmich na Michael Olise, lakini Flekken alifanya kazi kubwa kuzuia mabao zaidi, huku Leverkusen wakijaribu kujibu kupitia Nathan Tella na Patrik Schick bila mafanikio.
Kocha wa Bayern Vincent Kompany alisema “Tulichocheza kwa nidhamu na nguvu kubwa. Kufika fainali ni hatua muhimu, lakini bado kazi haijaisha.”
Katika dakika za mwisho, Luis Díaz alifunga bao la pili kupitia shambulizi la kushtukiza lililoanzishwa na Leon Goretzka, na kuthibitisha ushindi wa Bayern ambao sasa wanaendelea kuwania treble msimu huu.
Kwa upande mwingine, Leverkusen wameendelea kukosa mataji makubwa baada ya kushindwa tena kufuatia mafanikio yao ya zamani, huku mashabiki wakisubiri kurejea kwa enzi ya ushindi.

