Serge Gnabry Kukosa Kombe la Dunia Baada ya Jeraha la Paja

Mshambuliaji wa klabu ya Bayern Munich na timu ya taifa ya Ujerumani, Serge Gnabry, ametangaza kuwa hatoshiriki kwenye Kombe la Dunia la 2026 kutokana na jeraha la paja, akisema ndoto yake ya mashindano hayo imefikia mwisho.

Serge Gnabry Kukosa Kombe la Dunia Baada ya Jeraha la PajaGnabry alithibitisha taarifa hiyo kupitia mitandao ya kijamii, akieleza kuwa amepata majeraha ya Paja yatakayomuweka nje kwa muda mrefu, hatua iliyothibitishwa pia na klabu yake Bayern Munich.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Alisema “Siku chache zilizopita zimekuwa ngumu sana kuzichukulia. Msimu wa Bayern bado una mengi ya kupigania baada ya kutwaa ubingwa wa Bundesliga, lakini kwa upande wa ndoto ya Kombe la Dunia na Ujerumani, kwa bahati mbaya imeisha kwangu.”

Serge Gnabry Kukosa Kombe la Dunia Baada ya Jeraha la PajaNyota huyo wa zamani wa Arsenal aliongeza “Kama taifa lote, nitakuwa nikiwashangilia vijana wetu kutoka nyumbani. Sasa ni wakati wa kuangazia uponyaji na kurejea vizuri kwa maandalizi ya msimu ujao.”

Kocha wa Ujerumani Julian Nagelsmann amekuwa akimtegemea sana Gnabry katika kikosi cha taifa, ambapo mshambuliaji huyo ameifungia Ujerumani mabao 26 katika mechi 59 alizocheza.

Serge Gnabry Kukosa Kombe la Dunia Baada ya Jeraha la PajaTaarifa hiyo ni pigo kubwa kwa timu ya taifa ya Ujerumani, ambao walikuwa wakimtegemea katika mashindano ya kimataifa, huku mashabiki wakisubiri kuona namna timu itakavyokabiliana na pengo lake.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.