Newcastle Wafungua Mlango Kumuuza Yoane Wissa, Villa, Spurs na Forest Zatajwa

Klabu ya Newcastle United imeanza kufikiria kumuuza mshambuliaji Yoane Wissa katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi, huku Aston Villa, Tottenham Hotspur na Nottingham Forest zikiwa miongoni mwa klabu zinazofuatilia kwa karibu hali yake.

Newcastle Wafungua Mlango Kumuuza Yoane Wissa, Villa, Spurs na Forest ZatajwaWissa alijiunga na Newcastle kutoka Brentford kwa dau la pauni milioni 55 msimu uliopita, lakini ameonekana kushindwa kung’ara St James’ Park akifunga mabao matatu tu kutokana na changamoto za majeraha na kushuka kwa kiwango chake.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Kwa sasa, Newcastle wameripotiwa kuwa tayari kupokea ofa kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29, huku wakikubali kuwa huenda wakapata hasara kubwa ya kifedha kwani bei yake ya sasa ni chini ya nusu ya kile walicholipa.

Newcastle Wafungua Mlango Kumuuza Yoane Wissa, Villa, Spurs na Forest Zatajwa

Ripoti zinaeleza kuwa Wissa naye yuko tayari kuanza ukurasa mpya katika maisha yake ya soka, akihitaji muda zaidi wa kucheza kikosi cha kwanza mara kwa mara, jambo linaloweza kumfanya atafute uhamisho nje ya Uingereza.

Newcastle Wafungua Mlango Kumuuza Yoane Wissa, Villa, Spurs na Forest ZatajwaAkizungumzia hali hiyo, chanzo cha habari kimesema “Yoane Wissa anataka nafasi ya kucheza mara kwa mara, na yuko tayari kwa changamoto mpya msimu ujao.”

Klabu za Aston Villa, Tottenham na Nottingham Forest ziliripotiwa kumfuatilia hata kabla ya kujiunga na Newcastle, na sasa zimepewa taarifa rasmi kuhusu uwezekano wa kumpata katika dirisha lijalo la usajili.

Newcastle Wafungua Mlango Kumuuza Yoane Wissa, Villa, Spurs na Forest ZatajwaPia kuna uwezekano mkubwa wa Wissa kuhamia Saudi Arabia iwapo hakutakuwa na makubaliano ndani ya Premier League, huku Newcastle wakiendelea kupanga mabadiliko makubwa ya kikosi kutokana na changamoto za kifedha na matokeo yasiyoridhisha msimu huu.

 

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.