Baada ya kutoboa kwenda robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, Tottenham wanataka kurejea kwa kishindo kuendeleza jalamba la ushindi huku kwenye Ligi Kuu wakati wakikutana na Southampton pale dimbani St. Mary Jumamosi hii. Bila shaka, hapa pana kikosi bomba kitakachomvaa Southampton.
Katika gemu 3 za mwisho za Ligi Kuu Spurs hawajafanikiwa kushinda gemu yeyote, hii inawafanya waendelee kusua sua kujihakikishia nafasi ya kutwa taji hilo huku kukiwa na ushindani mkubwa zaidi kutoka kwa Liverpool na Manchester City waliopo kileleni, bila kusahau Man U naye anakuja kwa kasi tu.
Hatahivyo, wakali hawa wamefanya vyema sana katika gemu yao dhidi ya Dortmund wakiwa ugenini na kujihakikishia uhai wa ndoto yao kuelekea kutwaa taji la mabingwa. Hata hivyo mchezo wao umekuwa ishara kama wanaweza kurudi vyema zaidi kwenye Ligi Kuu pia.
Kwa Upande wa Southampton, wao wanafanya jitihada zaidi kujiondoa kwenye mtari mwekundu wa kushuka daraja wakisaka kuendelea kuwepo kwenye ligi hii.
Bila shalka vijana wa Ralph Hasenhuttl wanahitaji kuwekeza jitihada zao zote kwenye gemu hii na zingine zinazofuata ili wajihakikishie kusalia kwenye ligi pamoja na kupandisha nafasi za juu kabisa.
Mpangilio wa kikosi.


aisha
Safi sana taarifa njema
Furahav
Habari nzuri.
Povel
Habar njema