Stori kali kwa wapenda soka wa Hispania sasa ni nani atakuwa meneja wa Real Madrid kuchukua nafasi ya Santiago Solari? Wadau wengi wamekuwa wakimpa nafasi sana aliyekuwa meneja wa Manchester na kutimuliwa mwishoni mwa Jana. Tunaweza kusema kinachobamba mtaani kwa sasa ni ukaribu wa Jose kuuchukua Madrid umeneja klabuni hapo.
Kwa mujibu wa dondoo za mtaani mashabiki wanadai kurejea kwa Mourinho ambaye alishawahi kuwa meneja wa klabu hii kati ya mwaka 2010 na 2013 na kufanikiwa kushinda taji la La Liga mwaka 2012.
Kibarua cha meneja wa sasa inadaiwa kuwa kipo mashakani baada ya kushidnwa kuwapa matokeo mazuri. Wiki iliyopita walitolewa kwenye copa de Rey na Barcelona, pia wamepokea kichapo cha bao 4-1 dhidi ya Ajax akiwa kwake huku wakiwa na matumaini finyu kabisa ya kutwaa taji msimu huu.
Hata hivyo, ukiacha Mourinho ambaye anahusishwa sana kwa kipindi hiki ambacho hana kazi, meneja wa sasa wa Tottenham pia yupo kwenye orodha ya pili kwa ukaribu wa kupewa nafasi zaidi kama anaweza kukinasa kibarua hicho akifuatiwa na Antonio Conte anayetajwa kuwa kwenye nafasi ya tatu!


Zeiyana
Hitakua vizuri kama leal Madrid watampa ukocha mourhno