Wachezaji Wenye Majina Magumu na Marefu

 

Kwa takwimu zinazoishi, mpira wa miguu ni mchezo ambao unafuatiliwa sana duniani iwe ni kwa kuangaliwa au kuwa na mashabiki wengi. Ni mchezo ambao unafuatiliwa na zaidi ya watu milioni 265 na idadi hiyo inakua kadri siku zinavyosonga mbele. Leo tumekusogezea baadhi ya majina ya wachezaji ambayo kuyatamka kwake kunahitaji jitihada.

Cameron Borthwick-Jackson

Ni miongoni mwa majina marefu yanayopatikana duniani. Alijiunga na United tangu akiwa na umri wa miaka 6. Alibahatika kupandishwa katika kikosi cha timu ya kwanza kipindi cha Van Gaal lakini baada ya ujio wa Jose alimshusha na kumtoa kwa mkopo Wolves baadaye Leeds na sasa yupo Scunthorpe.

Pierre-Emerick Aubameyang

Miongoni mwa wachezaji wanaoiwakilisha Afrika kimataifa. Raia huyo wa Gabon anakaa katika kundi la wachezaji wenye majina magumu na marefu kwenye soka, ambapo utamkaji wa jina lake mara nyingi unahitaji uelewa na umakini mkubwa. Amecheza katika klabu nyingi kubwa kama Arsenal na Dortmund.

Sotiris Papagiannopoulos

Mchezaji huyu raia wa Sweden pamoja na kwamba jina lake ni refu lakini kinachofurahisha zaidi ni ugumu uliopo katika kulitamka jina hilo. Mtangazaji mmoja wa Uingereza aliwahi kufurahisha umma baada ya kushindwa kulitaja jina hilo na kuamua kuguna kwa baadhi ya sehemu.

Mohamed Lamine Zemmamouche

Mchezaji raia wa Algeria ambaye jina lake kiuhalisia ni refu sana na kuna walakini wakati wa kulitaja. Ni chaguo la pili ndani ya kikosi cha Algeria japo hajapata wakati mwingi kukaa katikati ya milingoti miwili, lakini anakaa katika historia hiyo.

Jakub Błaszczykowski

Raia huyo wa Poland ni miongoni mwa wachezaji ambao majina yao yanahitaji uelewa mzuri wa asili ya taifa hilo. Ni jina ambalo sio rahisi kwa mtu kulitaja. Hata watangazaji wamekuwa wakipata ugumu kulitaja jina hilo zaidi wamelifupisha na kumwita ‘Kuba’ ili kurahisisha utamkaji.

Jan Vennegoor of Hesselink

Mchezaji huyo wa zamani wa Celtic na mshambukiaji wa Hull, jina lake ni miongoni mwa majina yanayofurahisha sana katika karne hii kutokana na urefu wake na baadhi ya sehemu kuwa na ugumu kuzitamka. Jina lake lina muunganiko wa familia zake zote mbili na kulifanya kuwa refu sana hata kulitamka na wakati mwingine huwapa ugumu watangazaji.

 

3 Komentara

    Majina marefu sana

    Jibu

    Habar njema

    Jibu

    Hatari sana mtu anajina refu kama nn!!!#meridianbettz

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.