Kizazi cha Dhahabu Afrika

Nyota wengi wa Kiafrika wanapopata nafasi ya kusalia ndani ya ligi fulani na kuaminiwa kwa hakika hutumia nafasi hiyo kuthibitisha imani mbele ya waliojenga uaminifu kwao. Baadhi ya wachezaji wenye asili ya Afrika na wanacheza na timu zao za taifa Afrika ndiyo tunaowaangazia sana jicho.

Kutoka kwenye Uafrika wao hadi ngazi ya dunia ambako kwa hakika wameweza kushinda kiatu cha dhahabu ambacho ni heshima kubwa sana ndani ya ligi kutokana na uwezo wa kufunga magoli mengi ndani ya msimu mmoja wa ligi husika jambo ambalo hutambuliwa kwa kuzawadiwa kiatu cha dhahabu ambacho ni ishara ya pekee.

Msimu huu ulikuwa wa kipekee sana ndani ya ligi ya Uingereza kutokana na kushuhudia nyota watatu wa Kiafrika wote wakiwa na idadi sawa ya magoli kwenye ligi wanazochezea huku wawili wakitoka katika klabu moja. Hii ni dalili kubwa sana ya ukomavu wa soka la Afrika kutokana na makubwa yanayofanywa na vijana hao. Baadhi ya nyota ambao wana historia hiyo kwenye historia ya sola la Uingereza ni kama vile:

Didier Drogba (Ivory Coast), alishinda kiatu hicho mara mbili akiwa na klabu ya Chelsea. Msimu wake wa kwanza kushinda ilikuwa ni ule wa 2006/07 ambapo alifikisha jumla ya magoli 20 akiwapiku nyota wengine wote ndani ya msimu huo. Msimu mwingine wa nyota huyo kushinda ni ule wa 2009/10 ambapo alifikisha jumla ya magoli 29. Kwa nafasi yake katika klabu yake hiyo yeye ndiye mchezaji ambaye ana historia nzito ndani ya klabu yake hiyo akiwapa mataji ya ligi mara mbili mfululizo, 2005 na 2006; pia akawapa kombe la klabu bingwa mwaka 2012.

Pierre Emerick Aubameyang (Gabon), ameng’ara katika klabu zote alizoweza kupitia ikiwemo Borussia ambako amecheza kwa mafanikio makubwa sana. Pia, ana msimu wenye mafanikio makubwa ndani ya Arsenal baada ya kutwaa kiatu hicho na kuwafikisha kwenye michuano ya Europa hatua ya fainali. Naye amekuwa chambo cha mafanikio ndani ya klabu hiyo huku akinyakua kiatu hicho cha dhahabu ndani ya ligi hiyo.

Sadio Mane (Senegal), alijiunga na Liverpool 2016 na hadi sasa amekuwa na mchango mkubwa sana katika klabu hiyo. Pia, amepata tuzo ya kiatu hicho. Magoli yake yamepatikana bila penati yoyote huku akitoa pasi za magoli pia.

Mohamed Salah (Misri), raia wengi wa taifa analotokea walijiunga kuishangilia klabu hiyo mara baada ya nyota huyo kujiunga na miamba hao. Na hakika hajawaangusha kutokana na mchango wake aliouonesha ndani ya klabu hiyo. Pia, amenyakua kiatu cha dhahabu ndani ya ligi hiyo pia.

2 Komentara

    Mane hadi sasa amekuwa na mchango mkubwa sana katika klabu yake ya Liverpool#meridianbettz

    Jibu

    Didier Drogba alikuwa na aliipa mafanikio makubwa Chelsea kushinda premier mara 2 na UEFA mara 1#meridianbettz

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.