Tetesi za Usajili

Winga wa Manchester City Leroy Sane, 24, yupo karibu kutua Bayern Munich kwa dau £70m.

Vilabu vya Premier League vitakutana Ijumaa kujadili kama msimu utamalizika kabla ya Juni 30. Kama itapigwa kura, vilabu 14 kati ya 20 vinatakiwa vikubali. (Guardian)

Barcelona wanataka kumsaini kuingo wa Chelsea na France, N’Golo Kante, 29. The Blues wanaweza kuamua kubadilishana na Mbrazili Philippe Coutinho, 27, ambaye kwasasa yupo Bayern Munich kwa mkopo akitokea Barca.

Chelsea wamevutiwa mkusaini nahodha wa AC Milan na Italy beki wa kati Alessio Romagnoli, 25.

Straika wa Chelsea na France, Olivier Giroud, 33, yupo tayari kupunguza mshahara wake ili kuhakikisha anatua Inter Milan kipindi cha kiangazi.

Beki wa Manchester United na Argentina, Marcos Rojo, 30, anataka kuongeza mkataba wake wa mkopo katika nchi yake akiwa Estudiantes baada ya kucheza mchezo mmoja na kupata majeruhi na ligi kusimamishwa kwasababu ya Corona.

AC Milan wameamua kutokuweka ofa kumnasa kiungo wa Uingereza Adam Lallana kipindi hiki cha kiangazi. Mchezaji huyo wa zamani wa Southampton, 31, mkataba wake unamalizika mwishoni mwa June.

Arsenal wanaweza kumuuza staika wake Alexandre Lacazette mwishoni mwa msimu, wakati Atletico Madrid wanamtaka mchezaji huyo.

Alexandre Lacazette

Japo, Arsenal inaweza kumpoteza straika wake wa Gabon, Pierre-Emerick Aubameyang, ambaye anatakiwa na Real Madrid. Zinedine Zidane anamtaka kama mbadala wa mshambuliaji wa Inter Milan, Lautaro Martinez ambaye anahitaji kuondoka Italia kwenda Barcelona.

Arsenal wanakaribia kukamilisha uhamisho wa beki wa kushoto wa Ufaransa Layvin Kurzawa wanakamilisha ada ya uhamisho kutoka PSG.

Arsenal wapo kwenye mazungumzo kumsain beki wa kati wa Reims na Ufaransa Axel Disasi, 22.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.