Bora Ningecheza na Roy Keane na Paul Scholes - Bruno Fernandez

Bruno Fernandes amesema anatamani angecheza na wakongwe wa Manchester United Roy Keane na Paul Scholes na ana amini utatu wao ungekua ni moto wa kuotea mbali. Fundi huyo wa mpira mwenye asili ya Kireno amewavutia mashabiki wengi wa Old Trafford baada ya kucheza vema na kuchagulia kama mchezaji bora wa mwezi wa pili mapema tu kabla ya kusimamishwa kwa michezo.

Bruno Fernandez

Anafahamu vema pia historia yake na manchester kwajivyo alivyo ulizwa na mashabiki hao kwa njiia ya mtandao kuhusiana na Keane na Scholes na yeye akagoma kuchagua mmoja wao na kusema angecheza na wote angetengeneza muunganiko bora sana.

“kwangu nikiwa na wote wawili itakua poa sana kwa maana nahitaji mshambuliaji wa kati anaeweza kuwafukuza mabeki mbele yake na kupiga pasi safi kama Keane na kuleta mipira iliyo hai kwangu kama mshambuliaji wa mwisho”

Bruno Fernandez amehamia Manchester akitokea sporting Lisborn ambako alifunga magoli 23 katika mechi 38 alizocheza na kuwafanya Manchester united kuvutiwa nae na kumsajiri kwa ada ya pauni milioni 55 mwezi january mwaka huu.

 

 

2 Komentara

    Uko sahii,mana hao watu wanatisha.

    Jibu

    Ipo Sikh utakutana nae

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.