Historia Uwanja wa Santiago Bernabeu Katika Jiji La Madrid

Mwanzoni mwa Karne ya 20 timu ya Real Madrid ilicheza kwenye viunga ambavyo kwa kipindi hicho ilikua ni kama kiwanja cha mchangani hapo Campo De O’Donnell na baadae kwenda kwenye kiwanja kikubwa kiasi cha Campo de Chamartín mwaka 1924. ilipofika mwaka 1943 uwanja wao ukawa mdogo tena hivyo aliyekua Raisi wa timu hiyo bwana Santiago Bernabeu akataka Madrid iwe na uwanja wa watu 100,000/=

Uwanja wa Santiago Bernabeu miaka ya1929

Uwanja huo ulipaswa kujengwa pale pale Campo de Chamartin . Na uwanja huo uliendelea kupewa jina hilo hilo la Campo de Chamartin mpaka baada ya miaka nane kupita ndipo ukapewa jina la Santiago Bernabeu.

Kwa wakati huo uwanja wa Santiago Bernabeu ulikua unaweza kubeba watu 75,000 tu na uliongezewa uwezo wa kubeba waudhuriaji 125,000 mwaka 1954 baada ya upande mmoja wa majukwaa kuongezewa nafasi.

Kuelekea miaka ya 1970 uwanja ulianza kuchakaa na timu ikapendekeza uwanja kujengwa kaskazini mwa mji wa Madri, Lakini kutokana na uharaka wa kuendesha mashindano ya kombe la dunia kwa nchi hiyo la mwaka 1982 uwanja ulifanyiwa marekebisho ya kiasi na kupunguza idadi ya watu kufikia 90,800/=.

 

 

2 Komentara

    Habar njema

    Jibu

    Good news

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.