Chelsea haitaji wafanya kazi kufanya kazi siku za ziada bila malipo, wakati mechi zikirejea, lakini pia wamelipwa pesa kwaajili ya likizo. Chelsea wameamua kuwalipa wafanyakazi wake kwasababu wanahofia, mechi huenda zikacheza bila mashabiki.
Mwenyekiti, Bruce Buck, amenukuliwa kwenye tovuti ya klabu: “Sisi siku zote tumejidhatiti katika kusaidia jamii, hasa wahanga, na tunafikiri wakati huu ni vyema kufanya hivyo kuliko wakati wote.

“Mmiliki wetu, Roman Abramovich, amekuwa chachu yetu kutafuta namna ya kuwasaidia wenye uhitaji na baada ya kuanzisha kampeni ya wakimbizi na kufanya Millennium Hotel pale Stamford Bridge kutumiwa na NHS, hiki ni kipaumbele, natarajia kuona inatumika.”


Povel
Gud news