Luc Eymael Hataki Nyota wake Wanenepe

Kochwa wa Yanga, Luc Eymael amewataka nyota wake kuhakikisha wanajitunza kipindi hiki cha mapumziko na sio kunenepa. Amewataka nyota wake kufanya program ya mazoezi aliowapatia, pamoja na ligi kusimama kutokana na janga la Corona.
Nyota hao ni Lamine Moro, Bernard Morrison, Juma Abdul, Haruna Niyonzima, Ditram Nchimbi, Said Juma, Patrick Sibomana na Papy Tshishimbi ni wachezaji ambao wanatazamwa kwa uangalizi zaidi.
Bernard Morrison na Haruna Niyonzima
Mbeligiji huyu anataka kuhakikisha Wananchi wanabaki kwenye kiwango chao, pamoja na ligi kusimamishwa.

“Nafatilia maendeleo ya kila mchezaji akiwa nyumbani, kwasababu nataka timu iwe na muonekano mzuri mechi zikirejea,” Eymael amesema.

“Ninawatazama sana, Moro, Morrison, Juma, Niyonzima, Ditram, Said, Sibomana, na Papy kwasababu zangu za kiufundi. Nataka kuona wakifata maelekezo waliyopewa na benchi la ufundi. Lakini kila siku napata repoti ya kila mchezaji.”

“Tunataka watunze hali zao kisaikolojia na fizikia, haitafurahisha ukiwakuta wachezaji wanashepu mbaya. Timu inatakiwa iwe tayari kucheza muda wowote na ndio maana tunaendelea kujiandaa.”

Yanga kwasasa wapo nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi wakuwa na alama 51.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.