1. Tangu amejiunga na kikosi cha kwanza cha Barcelona amezifunga si chini ya goli 7 kila timu inayoshiriki ligi kuu ya nchi hiyo klabu ya Sevilla ndio inamtazama Lionel Messi kwa jicho la husuda baada ya kuifunga magoli 37 katika mechi 38 alizopata kucheza dhidi ya timu hiyo. Akiwa na Barcelona ameweza Messi kucheza dhidi ya timu 40

2. Gerald Pique mlinzi wa kati wa FC Barcelona ndio mchezaji ambaye Messi anamtaja kama mchezaji aliyecheza nae kwa muda mrefu pamoja . Huyu walianza soka pamoja pale FC Barcelona kwenye Academy yao ya La Masia . Mwaka 2004 alikwenda Manchester United akaichezea mechi 12 tu kabla ya kumtoa kwa mkopo Zaragoza . Mwaka 2008 alirudi FC Barcelona ambayo anaichezea mpaka sasa akiwa na Messi.
3. Kila anapofunga goli hunyoosha vidole vyake juu na pia hutazama juu. Wengi hawafahamu kwanini hufanya hivyo , hivi karibuni akifanya mahojiano na waandishi wa habari alisema humkumbuka bibi yake bi Celia ambaye alifariki mwaka 1998. Bibi huyo ndio aliyemlea Messi na kumwekea ndoto yakuwa mcheza mpira mkubwa licha ya changamoto za kiafya alizokuwa nazo . Bahati mbaya alifariki bila kuyaona mafanikio ya Messi.

4. Kwa kulelewa ndani ya jiji la Barcelona na kutumia maisha yake yote ya soka nchini Spain, Messi alikuwa na uwezo kisheria kuchukua uraia wa nchi hiyo na mwaka 2010 angevaa jezi za timu ya taifa ya nchi hiyo badala ya nchi yake asilia ya Argentina . Viongozi wa chama cha soka cha Uhispania walijaribu kumshawishi lakini aligoma na kuikumbuka nchi yake ambayo amesimama kama mfungaji wao wa muda wote akiwa na magoli 70 bila taji lolote .
5. Unamfahamu kocha wa timu ya vijana ya Argentina chini ya miaka 17 ? huyo ndio role model wa Lionel Messi si Diego Maradona . Pablo Aimar aliyekuwa kiungo mshambuliaji wa Benfica na timu ya taifa ya Argentina ambaye sasa ana miaka 40 ndio rafiki mkubwa wa Messi na ndie ambaye anamtaja kama ‘ Role Model ‘ wake katika soka. Pablo aliichezea Argentina mechi 52 na kufunga magoli 8 kuanzia mwaka 1999 hadi mwaka 2009.


Elika
Hongera kwake mess.asanten kwa habari njema mnazotupatia meridianbet