Mshambuliaji wa klabu ya Brescia na timu ya taifa ya Italia Mario Baloteli pengine kwa rekodi ya kuhesabika kua ni mmoja wa wachezaji watukutu zaidi kuwahi kutokea nchinni Italia kwa kipindi cha miaka 10 iliyopita.

Baloteli licha ya utukutu, ni mmoja wa wachezaji wenye kipaji kikubwa kiasi kuna kipindi ilikuwa inawekwa shinikizo kumuita kikosi cha timu ya Italia baada ya mara kwa mara kuwakasilisha makocha na wenzie kwa faulo zake zisizo na kichwa wala miguu lakini pia anatajwa kua na maisha ya kihuni nje ya soka.
Katika maisha yake ya soka amepata kuvichezea vilabu vingi katika ligi mbalimbali duniani lakini hivi karibuni ameizungumzia klabu ya Manchester City na ligi ya England kama kwake ni klabu bora na ligi bora kuwahi kuichezea.
“ nikiwa England watu walikuwa wananiona mwehu, ndio kichaa kabisa binafsi nasema ulikuwa utoto na ujana . Kwangu EPL ni ligi bora na pia maisha ndani ya Manchester city yalikua bora sana na kwa sasa nikitafakari naona ilikuwa sehemu salama. Kuna kitu nilipoteza pale ila sijui ni nini, najutia muda mwingine lakini mwisho wa yote ulikuwa ujana na si ukichaa”
Huyo ndio Baloteli ambaye daima humtaja Jose Mourinho kama kocha bora kwake.

