Chanzo cha habari cha Italia kimeripoti kuwa nyota Gonzalo Higuain anaweza kuamua kuchelewa kurejea Juventus au kutorejea kabisa klabuni hapa. Taarifa hii inataja kuwa staa huyu anahitaji kuwa karibu na mama yake ambaye ni mgonjwa.
Staa huyu alikuwa wa kwanza kabisa kuondoka Italia baada ya kuanza rasmi kwa zuio la kutoka nje na kukaa karantini, hii ilikuwa ni baada ya Paulo Dyabala, Daniele Rugani na Blaise Matudi kupatikiana na maambukizi ya virusi vya Corona.
Higuain aliruhusiwa kusafiri baada ya siku 14 za kuwa Karantini akisafiri kuelekea Argentina. Mama yake Higuain yupo nchini Argentina akipambana na Kansa.
Nchi ya Italia inatarajiwa kuanza kuruhusu shughuli zote za kila siku angalau kuanzia mwezi mei, hivyo vilabu tayari vinaanza kuwasilina na wachezaji wao kwa ajili ya kurejea ili waweze kukaa karantini kwa siku 14 kabla ya kumalizia sehemu ya msimu iliyobaki.
Hata hivyo, taarifa inataja kuwa staa huyu yeye haoni kama ni wakati muafaka wa kuwahi kurejea Italia, ukiacha suala la janga la corona bado anahitaji kuwa pamoja na mama yake katika kipindi hiki kigumu ambacho mama yake anapambana na kansa.

