Anthony Joshua amewatupia neno mabondia wengine Dillian Whyte na Oleksandr Usyk kuwa wapo kwenye orodha ya watu anaotaka kukutana nao ulingoni.
Siku kadhaa zilizopita AJ alionesha nia ya kutaka kupambana na Tyson Fury akidai kuwa haiwezekani kukawa na mabingwa wawili wa dunia. AJ anadai kuwa Fury hastaili kuitwa bingwa wa dunia, mpaka pale watakapokutana na yeye.
AJ Anaonekana kuwa amedhamiria kupambana na manguli wanaotamba kwenye ndondi na ameendelea kutoa orodha ya watu anaotaka kupanda nao ulingoni. Safari hii amesema kuwa anataka kukutana na watu wagumu kama Dillian Whyte na Oleksandr Usyk.
White amekuwa akimchana Anthony Joshua kuwa aache kujifanya kama alikuwa anataka pambanbo na yeye maana alichagua pambano jingine la USA. Wakati upande wake Johsua amesema anatambua kuwa white amekuwa akifukuzia ubingwa wa dunia, na alimpa nafasi hiyo mwezi Aprili mwaka jana akaikataa.
Joshua anashikilia ubingwa wa WBA, IBF, na WBO wakati Fury akishikilia ubingwa wa WBO. AJ anamtaka Joshua ili ajiite namba 1 akutane neye ulingoni, kisha akutane na hao wengine waliopo kwenye orodha yake.
Furahav
Wazichape tuone nani atashinda.