Kiungo wa klabu ya Chelsea, Jorginho “anafurahiwsana” na maisha kwenye Klabu hiyo ya London na hakuna “chochote” kuhusu Mazungumzo ya kuhamia Juventus, wakala wake amesisitiza.
Mchezaji huyo wa Kimataifa wa Italia mwenye umri wa miaka 28 amehusishwa na kuungana tena na kocha wake, Maurizio Sarri huko Turin baada ya miaka miwili na The Blues, ambapo alimsajili kutoka Napoli, Lakini wakala wake Joao Santos amekanusha uvumi, na hata hivyo aligusia kuwa Jorginho anaweza kuongeza Mkataba wake huko Stamford Bridge.
“Juventus? Nilisoma hiyo, lakini sikuwahi kuwasiliana nao, “Wala Sarri wala Fabio Paratici hawajawahi kuniita kwa habari juu ya Jorginho. Hadi leo, sijui kabisa juu ya hali hii.

“Anafurahiya sana London, ambapo anaonyesha thamani yake na bado ana miaka mingine mitatu kwenye mkataba wake… Kwa kweli, mnamo Julai, kuna uwezekano wa kuongeza mazungumzo ya Kuongeza mwaka wa nne.. Ndio tutafungua mazungumzo ya mkataba mpya na Chelsea.
“Hatujui mikakati ya usajili wa Juventus ni nini, lakini hii ni mipango yetu kwa siku zijazo. Ninarudia, hadi leo, hakuna Juventus wala timu yoyote nyingine ambayo imejitokeza mbele.”.


Sadick
Anacheza pasi nyingi lakini hazina madhara kwa timu pinzani#meridianbettz
Fatina mfingi
Asnateh kwa taarifa #meridianbet