Szczesny Aeleza Sigara Ilivyomtimua Arsenal

Wojciech Szczesny amefunguka ukweli baada ya kukutwa anavuta sigara na ukawa mwisho wake wa kucheza soka Arsenal.

Szczesny aliwasha sigara baada ya kipigo cha 2-0 dhidi ya Southampton kipindi cha mwaka mpya, ilipelekea kupigwa faini na kuachwa na Kocha Arsene Wenger kama adhabu.

Kipa huyo wakimataifa wa Poland amekiri hakukuwa na sababu ya Wenger kumuacha kwani hakuonekana tena hadi kwenye mechi ya Kombe la FA.

Szczesny alienda kwa mkopo Roma kwa misimu miwili kabla ya kuuzwa jumla Juventus 2017 majira ya kiangazi, amekiri tukio hili lilimtoa kutoka chaguo la kwanza hadi kuondoka Arsenal.

“Kipindi ch nyuma nilikuwa navuta kila wakati na Kocha alikuwa anajua, hakutaka mtu avute kwenye vyumba vya kubadilishia nguo na nilifahamu hilo pia.”

“Kwasababu ya hali ya mchezo, nilivuta sigara wakati timu ikiwa ndani. Nilikwenda kwenye kona ya bafu, lilikuwa mwishoni mwa chumba cha kubadilishia nguo na hakuna wakuniona, nikawasha moja..

“Kuna mtu aliniona, wala hakuwa kocha mwenyewe, na aliripoti kwa kocha. Tulionana siku kadhaa baadae, aliniuliza kama ilikuwa kweli, nilijibu ndio. Alinipa faini na hapo ndio ilikuwa mwisho wangu.

“Baadae akasema, utakuwa nje ya timu kwa muda  lakini hakutakuwa na adhabu nyingine. Nilikuwa mtaalamu kwenye hili.

“Nilikuwa natarajia kurejea kwenye baada ya wiki kadhaa baadae, tulikuwa na mwendelezo mzuri na David Ospina, aliingia golini, alicheza vizuri kwa michezo michache. Aliendelea kucheza.

3 Komentara

    Sigara sio nzr kiafya.

    Jibu

    Duuuh

    Jibu

    Duhh

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.