"Kagere ni Hatari" Rajab Zahir

Beki wa Ruvu Shooting Rajab Zahir amechagua washambuliaji wawili ambao ukicheza nao lazima uwe nao makini dimbani. Zahir amekiri Meddie Kagere na Tariq Seif ndio washambuliaji hatari aliwahi kucheza dhidi yao.

Kagere, ni mchezaji wa Simba ambae pia ndio kinara wa magoli, ametajwa sana kuwa ni mwiba kwa mabeki.

“Meddie Kagere ni straika msumbufu wakati wote ukicheza dhidi yake, moja wenu lazima amtazame kwa karibu kila sekunde ya mchezo na kuhakikisha hapati nafasi, anakuwa mbaya sana akiwa kwenye nafasi.” Zahir

Zahir ameeleza kuwa kumkaba Seif lazima uwe makini kwa mmoja akimpatia nafasi ana nafasi kubwa ya kushinda.

“Angalia magoli anayofunga Tariq, unashtuka tu mpira upo wavuni, ukimsahau kuwa yupo uwanjani atakukumbusha kwa goli,”

 

“Mmoja lazima ahakikishe Tariq hapati nafasi ya kubaki na goli, kwani amefunga magoli mengi ya namna hiyo. Ni mchezaji mzuri lakini ni hatari akiwa mbele ya goli.”

Seif amekuwa na muda mchache wa kuonyesha kiwango chake akiwa Yanga kutokana na upinzani wa namba kutoka kwa Ditram Nchimbi, Gnamien Yikpe na David Molinga, ambao mara nyingi wamekuwa chaguo la kwanza kwenye kikosi.

Molinga, anaweza kuachwa kwenye kikosi cha wananchi, japo ndio kinara wa magoli mwenye magoki 8 kwenye timu.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.