Sevilla Yainyamazisha Manchester United.


Matumaini ya Manchester United kunyanyua ubingwa wa Europa League kwa mara ya pili chini ya kipindi cha miaka minne yalizimwa na Sevilla mnamo Agosti 16, 2020.

Hii ni baada ya miamba hao wa soka ya Uingereza kupokezwa kichapo cha 2-1 kwenye nusu-fainali iliyowakutanisha mjini Dusseldorf, Ujerumani.

Sevilla ambao ni mabingwa mara tano wa Europa League, walitoka nyuma na kusajili ushindi ambao uliwakatia tiketi ya kunogesha fainali itakayowakutanisha na mshindi nusu-fainali nyingine kati ya Inter Milan ya Italia na Shakhtar Donetsk ya Ukraine.

 

Sevilla Yainyamazisha Manchester United.

Nusu-fainali hiyo ya pili, ambayo pia itakuwa ya mkondo mmoja pekee, itachezewa nchini Ujerumani mnamo Agosti 17, 2020, siku nne kabla ya fainali kutandazwa Ijumaa ya Agosti 21.

Kiungo mzawa wa Ureno, Bruno Fernandes aliwaweka Man United kifua mbele kupitia penalti ya dakika ya tisa. Ni bao lililowapa ari zaidi huku wakionekana kuwazidi wapizani wao maarifa katika takriban kila idara.

Ingawa hivyo, Sevilla wananolewa na kocha Julen Lopetegui, walisalia imara huku kipa wao Yassine Bounou akifanya kazi ya ziada na kupangua makombora makali aliyoelekezewa na mfumaji Marcus Rashford aliyeshirikiana vilivyo na Fernandes na kiungo Paul Pogba.

Fowadi wa zamani wa Liverpool, Fernandez Saez ‘Suso’ Joaquin alisawazishia Sevilla katika dakika ya 26 baada ya kukamilisha krosi aliyopokezwa na Sergio Reguilon kwa ustadi mkubwa.

 

Sevilla Yainyamazisha Manchester United.

Luuk de Jong ambaye ni kiungo wa zamani wa Newcastle United, alikizamisha kabisa chombo cha Man United baada ya kufungia Sevilla bao la pili na la ushindi katika dakika ya 78.

Bao hilo lilitokana na utepetevu wa mabeki wa Man United walioshindwa kudhibiti vilivyo krosi iliyopigwa na nyota wa zamani wa Manchester City, Jesus Navas.

Sevilla walifuzu kwa nusu-fainali baada ya kuwabandua Wolves kwa 1-0 mnamo Agosti 11, 2020. Walifungiwa bao hilo na Lucas Ocampos.

Kwa upande wao, Man-United walitinga hatua ya nusu-fainali baada ya kuwapiga FC Copenhagen ya Denmark 1-0 kupitia penalti ya dakika za mwisho iliyofungwa na Fernandes.

 

Sevilla Yainyamazisha Manchester United.

Sevilla ambao kwa sasa wametinga hatua ya nusu-fainali ya Europa League mara saba, wanajivunia rekodi ya kunyanyua ufalme wa Europa League mara nyingi zaidi na wametawazwa mabingwa katika misimu yote mitatu ambayo imewashuhudia wakifika awamu ya robo-fainali.


Drops and Wins!

Umeijua hii? Ni promosheni kabambe ya ushindi kwenye Casino ya mtandaoni ya Meridianbet! Unaweza kushinda hadi Euro 2,000,000 leo.

Soma Zaidi

40 Komentara

    Hongeren Sevilla mmeonyesha ushujaa wenu kwa kuwafunga United.

    Jibu

    Na kwa taarifa yenu De Gea amefanya makusudi kachoka maana alikuwa anawaokoa sana lakini mwisho wa siku mnasema kiwango chake kibovu kwahiyo jana kasema isiwe tabu najirusha kama nafuata hivi kumbe naachia makusudi

    Jibu

    Hongera sana Sevilla kwa kuwafunga united#Meridianbettz

    Jibu

    Man ilicheza vzr sana ni kwamba haikuwa na bahati kwa kushindwa kutumia nafasi ilizopata kufunga magoli zaidi na Van Persie alitoa tahadhari mapema kwa man u kutochukulia kirahisi mchezo huo#meridianbettz

    Jibu

    Wanastahili pongezi za dhati.

    Jibu

    Ndio mpila ilikuwa akuna jinsi walifosi iliwapate ushindi lakini ndio ivyo imeshindikana

    Jibu

    Hongera kwake sevilla

    Jibu

    Sevilla hongera sana kwa kuonesha kipaji chenu maana sio powa wata hawajatarajia

    Jibu

    Kwa kweli man u haikuwa na bahata Jana mana walipata nafasi nyingi kufika kwenye lango LA Seville ila walianbulia patupu na kufungwa 2 ambayo ilikuwa faida ya Seville

    Jibu

    united mlijua kutupasua mioyo yetu jana ila hatuna namna maana katika soka kuna matokeo matatu

    Jibu

    Manchester haina bahati

    Jibu

    safi sevila mmejua kunifurahisha

    Jibu

    Sevilla anastahili pongezi
    @meridianbettz

    Jibu

    Safi Sevilla

    Jibu

    Mpira kweli unaduka kila MTU akutegemea kama man wanaweza kupigwa kwa timu ndogo kama sevilla hata hvyo man sasa HV wameshuka kiwango

    Jibu

    Sevilla game ilikuwa upande wao man walishambulia sana lakin bahat haikuwa kwao

    Jibu

    Daah man u bado.

    Jibu

    tena bado kabebwa hapo

    Jibu

    Kila mtu ana mbabe wake

    Jibu

    Hiyo gemu Manchester United waliidharau sana maana Kama nafas walipata nzur sana na walikuwa na nafas nzur ya ushind sema kudharau mechi ndo habar wakaipata maana Kama ukiangalia kiukwel hiyo gem Sevilla alibanwa sana pale alipopata nafas tu alionyesha uwezo wake kiukwelech ilikuwa nzur sana

    Jibu

    Hongera sana sevila

    Jibu

    Hongera Sana Sevilla

    Jibu

    Habari njema kwa mashabiki wa sevilla

    Jibu

    Good

    Jibu

    Matokeo yamekua yakushangaza Sana sivyo Kama watu walivyokua wakitabili ama kweli mpira unamatokeo ya ajabu Sana.

    Jibu

    Sevilla walikuwah kwny ubora Sana ile Jana congrat Sevilla fc

    Jibu

    Man U mmeniboa sana

    Jibu

    Man u wameua mkeka wangu niliwapa ushindi wamenikera

    Jibu

    Hongera sana sevilla

    Jibu

    Man u walicheza vizuri tu sema bahati haikuwa yao

    Jibu

    Sevilla Jeshi kubwa#meridianbett

    Jibu

    Maoni:daaaa tumeumia sana mashabiki wa man united

    Jibu

    Bao hilo lilitokana na utepetevu wa mabeki wa Man United walioshindwa kudhibiti vilivyo krosi iliyopigwa na nyota wa zamani wa Manchester City, Jesus Navas.

    Jibu

    Kwa matokea waliyo kua nayo Manchester united wana panda wana shuka hadi kuja kufikia nusu fainali ilikua kama bahati tu.

    Jibu

    Niljua tu Sevilla atashinda

    Jibu

    Man u tunamajonzii

    Jibu

    Waliwakomesha,

    Jibu

    kwa taarifa yenu De Gea amefanya makusudi kachoka maana alikuwa anawaokoa sana lakini mwisho wa siku mnasema kiwango chake kibovu kwahiyo jana kasema isiwe tabu najirusha kama nafuata hivi kumbe naachia makusudi

    Jibu

    Imeniuma sana

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.