Matumaini ya Manchester United kunyanyua ubingwa wa Europa League kwa mara ya pili chini ya kipindi cha miaka minne yalizimwa na Sevilla mnamo Agosti 16, 2020.

Hii ni baada ya miamba hao wa soka ya Uingereza kupokezwa kichapo cha 2-1 kwenye nusu-fainali iliyowakutanisha mjini Dusseldorf, Ujerumani.

Sevilla ambao ni mabingwa mara tano wa Europa League, walitoka nyuma na kusajili ushindi ambao uliwakatia tiketi ya kunogesha fainali itakayowakutanisha na mshindi nusu-fainali nyingine kati ya Inter Milan ya Italia na Shakhtar Donetsk ya Ukraine.

 

Sevilla Yainyamazisha Manchester United.

Nusu-fainali hiyo ya pili, ambayo pia itakuwa ya mkondo mmoja pekee, itachezewa nchini Ujerumani mnamo Agosti 17, 2020, siku nne kabla ya fainali kutandazwa Ijumaa ya Agosti 21.

Kiungo mzawa wa Ureno, Bruno Fernandes aliwaweka Man United kifua mbele kupitia penalti ya dakika ya tisa. Ni bao lililowapa ari zaidi huku wakionekana kuwazidi wapizani wao maarifa katika takriban kila idara.

Ingawa hivyo, Sevilla wananolewa na kocha Julen Lopetegui, walisalia imara huku kipa wao Yassine Bounou akifanya kazi ya ziada na kupangua makombora makali aliyoelekezewa na mfumaji Marcus Rashford aliyeshirikiana vilivyo na Fernandes na kiungo Paul Pogba.

Fowadi wa zamani wa Liverpool, Fernandez Saez ‘Suso’ Joaquin alisawazishia Sevilla katika dakika ya 26 baada ya kukamilisha krosi aliyopokezwa na Sergio Reguilon kwa ustadi mkubwa.

 

Sevilla Yainyamazisha Manchester United.

Luuk de Jong ambaye ni kiungo wa zamani wa Newcastle United, alikizamisha kabisa chombo cha Man United baada ya kufungia Sevilla bao la pili na la ushindi katika dakika ya 78.

Bao hilo lilitokana na utepetevu wa mabeki wa Man United walioshindwa kudhibiti vilivyo krosi iliyopigwa na nyota wa zamani wa Manchester City, Jesus Navas.

Sevilla walifuzu kwa nusu-fainali baada ya kuwabandua Wolves kwa 1-0 mnamo Agosti 11, 2020. Walifungiwa bao hilo na Lucas Ocampos.

Kwa upande wao, Man-United walitinga hatua ya nusu-fainali baada ya kuwapiga FC Copenhagen ya Denmark 1-0 kupitia penalti ya dakika za mwisho iliyofungwa na Fernandes.

 

Sevilla Yainyamazisha Manchester United.

Sevilla ambao kwa sasa wametinga hatua ya nusu-fainali ya Europa League mara saba, wanajivunia rekodi ya kunyanyua ufalme wa Europa League mara nyingi zaidi na wametawazwa mabingwa katika misimu yote mitatu ambayo imewashuhudia wakifika awamu ya robo-fainali.


Drops and Wins!

Umeijua hii? Ni promosheni kabambe ya ushindi kwenye Casino ya mtandaoni ya Meridianbet! Unaweza kushinda hadi Euro 2,000,000 leo.

Soma Zaidi

40 MAONI

  1. Na kwa taarifa yenu De Gea amefanya makusudi kachoka maana alikuwa anawaokoa sana lakini mwisho wa siku mnasema kiwango chake kibovu kwahiyo jana kasema isiwe tabu najirusha kama nafuata hivi kumbe naachia makusudi

  2. Man ilicheza vzr sana ni kwamba haikuwa na bahati kwa kushindwa kutumia nafasi ilizopata kufunga magoli zaidi na Van Persie alitoa tahadhari mapema kwa man u kutochukulia kirahisi mchezo huo#meridianbettz

  3. Kwa kweli man u haikuwa na bahata Jana mana walipata nafasi nyingi kufika kwenye lango LA Seville ila walianbulia patupu na kufungwa 2 ambayo ilikuwa faida ya Seville

  4. Mpira kweli unaduka kila MTU akutegemea kama man wanaweza kupigwa kwa timu ndogo kama sevilla hata hvyo man sasa HV wameshuka kiwango

  5. Hiyo gemu Manchester United waliidharau sana maana Kama nafas walipata nzur sana na walikuwa na nafas nzur ya ushind sema kudharau mechi ndo habar wakaipata maana Kama ukiangalia kiukwel hiyo gem Sevilla alibanwa sana pale alipopata nafas tu alionyesha uwezo wake kiukwelech ilikuwa nzur sana

  6. Bao hilo lilitokana na utepetevu wa mabeki wa Man United walioshindwa kudhibiti vilivyo krosi iliyopigwa na nyota wa zamani wa Manchester City, Jesus Navas.

  7. kwa taarifa yenu De Gea amefanya makusudi kachoka maana alikuwa anawaokoa sana lakini mwisho wa siku mnasema kiwango chake kibovu kwahiyo jana kasema isiwe tabu najirusha kama nafuata hivi kumbe naachia makusudi

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa