Baada ya kutolewa katika hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Europa. Nahodha wa Manchester United – Harry Maguire hakubaliani na uwezo wa timu yake.
Man United walipata goli la kuongoza kupitia mkwaju wa penati uliopigwa na Bruno Fernandez kabla ya Sevilla kusawazisha na kuongeza goli la pili. Goli kipa wa Sevilla – Bounou , anakila sababu ya kupewa pongezi kwa kuzuia nafasi kadhaa za magoli na kuwatoa kabisa Man United katika michuano hiyo.

Akizungumza na BT Sports baada ya mchezo huo, Maguire amenukuliwa akisema ” kufungwa hakukubaliki. Kuishia hatua ya nusu fainali hakukubaliki. Kushinda mataji kunakaribia, tunahitaji kushinda mataji.
“Timu bora imefungwa, wametuhukumu kwa nafasi tulizokosa. Tumefungwa kwa kona mbili kitu ambacho sio sahihi. Tulicheza vizuri na kustahili ushindi, tumeishia hatua ya nusu fainali kwa mara ya tatu msimu huu. Pengine ukosefu wetu wa uzoefu umetugharimu, tusingefungwa zile kona mbili.”

Kocha wa Manchester United – Ole Gunnar Solskjaer amenukuliwa akisema ” Inahuzunisha, ni ngumu kukubali. Tumecheza vizuri na kutengeneza nafasi lakini hatukupata matokeo tuliyoyahitaji.
“Tunahitaji kuboresha kikosi chetu, siwezi kusema lini au kama tutasajili lakini tunaliangalia hilo. Tunapaswa kuwa na uhakika wa 100% katika kutekeleza hilo.”

Kwa kupoteza nafasi ya kucheza Fainali ya Europa msimu huu. Sasa ni rasmi Manchester United wanamaliza msimu wakiwa wamecheza nusu fainali tatu bila ushindi. Katika Ligi Kuu Uingereza – EPL, Man United wamemaliza katika nafasi ya 3, pointi 33 nyumba ya vinara Liverpool.
Drops and Wins!
Umeijua hii? Ni promosheni kabambe ya ushindi kwenye Casino ya mtandaoni ya Meridianbet! Unaweza kushinda hadi Euro 2,000,000 leo.


Neema
Asante Kwa kutujuza #meridianbet
Ester jackson
Wazee wa penalty sasa wanaaza kulalamika kubalini tu kuwa mmetolewa mana kama kufunga mngefunga sana kipindi cha pili mlikuwa mnapata nafasi sana Ila haikuwa bahati yenu .waacheni Seville nao wakafike nusu fainali bahna .ha ha haaa .
Tatu
Hizo ni kauli za kishujaa man sasa wameshashuka kiwango chao cha uchezaji
Ernest
Maguire kavurugwa na kipigo kona moja tuu jana
Sadick
Washambuliaji wanasitahili lawama ktk hili kwa kutotumia ipasavyo nafasi walizopata na walinzi kushindwa kulinda lango vema. Robin Van Persie alitoa tahadhari mapema kwamba Man Utd ijizatiti kwa kuchulia mchezo kwa umakini mkubwa. Ijipange msimu ujao #meridianbettz
Ernest
Hapa Maguire ameongelea kona mbili kanivuruga kamaanisha magoili mawili kupitia kona kama mpira wa adhabu baada ya kutoa nje mpira eneo la pembeni upande wa goli lao au Kona mbili akimaanisha pande mbele tofauti?? Amenivuruga ujue
Warda
Imeniuma sana hii ya Man kutoka daaa#Meridianbettz
Lydia Emmanuel Magoti
Ndio mchezo wakubaliane nahali Ila Man U wameniumiza Sana kwakipigokile
Latifa juma mohamed
United wamecheza vzr Lin hawakupata matokeo wanayohitaji poleni Sana man u
aisha
Hapo hainahaja ya kulalamika sana kinachotakiwa ni kujipanga upya
Mwanahamisi
Daah kweli inauma sana man kutoka
Adelta
Wajipange upya
@meridianbettz
magdalena
hatuna budi kuyapokea matokeo tunabidi tujipange upya na kuongeza juhudi united kwa ajili ya msimu ujao
Mwajumah
Duuh kweli inauma hii ya man kutoka#Meridianbettz
Fatina mfingi
Mmh
felister
poleni sana ila hii kwa game nilijua tu Kama man u watafungwa
Shan
Asiye kubali kushindwa sio mshindani ndo matokeo ya mpira.
Khadija
jamani inauma sana man kutoka
marry
izo ni changamoto za michezo
Issa
United ijipange san msimu ujao
Furahav
Ni kweli inauma sana.
Gabriel
Manchester United msimu huu wajipange wasajil wachezaji wazur wawauze wazee hao
Salma ngende
Aikuwa bahat yao
Fatuma kasomo
Nimoja ya changamoto
farida ahmadi
Ndio mpira huo haikuwa bahati kwa Manchester United
Genia Sikaluzwe
Ni vema wakajipanga upya
Janeflora malisa
Changamoto hizo
Shafii
Mpira unamatokeo matatu ushindi,sare na kupoteza na wahenga wana sema asiye kubali kushindwa si mshindani.
Povel
Ndo mpr wa miguu huo huna matokeo matatu na asiyekubal kushindwa si mshindani
Hope mwaikuka
Dk90
Sabrina
Hakuna jipya hapo
Devotha
Haikuwa riziki yao wamekosa makombe yote msimu huu duu!
JULIANA
Asante kwataharifa
Johnmary joel
Hongera juhudi sana iliuweze kufika unapo pataka#meridianbett
Nasra
Mashabiki wa Man u poleni
Flomena
“Timu bora imefungwa, wametuhukumu kwa nafasi tulizokosa. Tumefungwa kwa kona mbili kitu ambacho sio sahihi. Tulicheza vizuri na kustahili ushindi, tumeishia hatua ya nusu fainali kwa mara ya tatu msimu huu. Pengine ukosefu wetu wa uzoefu umetugharimu, tusingefungwa zile kona mbili.”
Zeiyana
Man Chester united walijitaidi sana ila ndio ivyo tena bahati haikua kwao..!
Caroline
Ni vizuri kukubali matokeo
Tahiya
Bahati haikuwa yenu man united mjipange mwakani
Saupha mohamed
Tukubali tu matokeo
Samiah
Ngojatuone hiyo dk90
David Pere
Maguire kavurugwa na kipigo kona moja tuu jana