Nahodha wa Montpellier, Vitorino Hilton aliweka historia ya kuwa mchezaji wa kwanza baada ya miaka 64 mwenye umri wa zaidi ya miaka 43 kusakata soka ya Ligi Kuu ya Ufaransa (Ligue 1).
Hii ni baada ya sogora huyo mkongwe kuwa sehemu ya kikosi cha Montpellier kilichowapepeta Olympique Lyon 2-1 mnamo Septemba 15, 2020.

Hata hivyo, alionyeshwa kadi nyekundu mwishoni mwa mechi hiyo kwa utovu wa nidhamu. Kosa lake lilichangia penalti iliyofungwa na fowadi wa zamani wa Manchester United, Memphis Depay katika dakika ya 82.
Hilton ambaye alifikisha umri wa miaka 43 mnamo Septemba 13, amekuwa akisakata soka barani Ulaya tangu 2002.
Mabao yote mawili ya Montpellier ambao kwa sasa wanashikilia nafasi ya tano jedwalini, yalifungwa na Teji Savanier katika dakika ya 38 na 59 mtawalia.

Ushindi kwa Lyon ungaliwakweza kileleni mwa jedwali la Ligue 1 ila wakajipata wakimaliza mechi na wachezaji 10 pekee uwanjani baada ya kiungo Houssem Aouar anayehusishwa pakubwa na Arsenal kuonyeshwa kadi nyekundu kunako dakika ya 44 kwa hatia ya kumchezea visivyo kiungo Arnaund Souquet.
Kufurushwa kwa Hilton na Aouar kunamaanisha kwamba jumla ya kadi 20 za rangi nyekundu zimetolewa hadi kufikia sasa kwenye soka ya Ligue 1 tangu mwanzoni mwa msimu huu wa 2020-21.
SHINDA NA MERIDIANBET!
Tengeneza pesa kidijitali kwa kubashiri mbio za farasi hapa Meridianbet! Chagua nani ashinde, unakusanya mkwanja.


Ester jackson
Duuh hatari sana miaka yote hiyo na bado ananguvu ya kuipambania timu sio mchezo jamani
Sauda
Kazi na umri..
Genia Sikaluzwe
Hongera Sana jamaa kwa kazi nzuri
Angelina
Yuko vizuri
felister
yuko vizuri
Adelta
Anastahili pongezi kwake@meridianbettz
Elika
Pongez kwake
Dorophina
Hilton yupo vizuri ingawa umri umeenda lakini bado ananguvu za kutumikia klabu yake
Zeiyana
Hilton hanajituna sana kwa umri alio kua nao hitachukua mda sana kustaafu
Fatina mfigi
Yupo vizur bado ila kazi na umri hilton!
Tatu
Umri wake mkubwa lakini bado yupo fiti
Mwanahamisi
Yuko vizuri
Sylvester
Mkongwe kazini
Caroline
Duhh kweli mkongweee
Tumaini kasalile
Naam kweli anastahili pongezi kwake
Mwajumah
Yuko vizur#Meridianbettz
Shani
Ukogwe katika kazi na kujituma kwake!!
Lydia Emmanuel Magoti
Mzee wakuli sakata kabumbu mkongwe bado anadai
Zahara omary
Mkongwe kazini
Theckla
Kweli ng’ombe hazeeki maini
Ernest
Hilton kibibi kizee cha Montpellier
Revina
Namba ya umri inasoma lakini kipaji hakipotei mzee piga kazi
Nasra
Kipaji hakipotei
Khadija
Kazi na umri#meridinbettz
Sabrina
Old is gold
Gabriel
Kwan ajui kuwa kazi na umri
Saupha mohamed
Yupo vizuri japo umri umeenda
aisha
Hilton yuko vizuri sana
marry
vizr
Johnmary joel
Anatambua wajibu wake ndomaana kawa mkongwe#meridianbett
Samiah
Safi kjn
Mariam mtandama
Yupo vizur
lombo
saf
Janeflora malisa
Nice
Fatuma kasomo
Ila yupo vizuri
Neema
Japo kazii na umrii ila km nguvu bado zipo na anaonyesha umahiri wake aendelee
Amiri Kayera
Amejitahid kulinda kiwango chake
Shafii
Anastahili pongezi hadi hapa alipofikia.
David Pere
Namba ya umri inasoma lakini kipaji hakipotei mzee piga kazi
Povel
Congrat kwake
Rose kapinga
Kweli ngombe hazeeki maini,piga kazi kama nguvu bado ipo umri namba tuu zisikutishe!!
magdalena
uyu jamaa ni noma yupo vizuri sana anajua mpira sana
Genia Sikaluzwe
Hongera Sana jamaa kwa kazi nzuri
Njiku
Ipo poa hii asante
Latifa juma mohamed
Ule usemi ya kwamba ng’ombe hazeeki maini.
Hopemwaikuka
Nc
Issa
Rekod nzuri bado mwili upo poa