Lwandamina : Tutapambana Mchezo Dhidi ya Simba.


George Lwandamina, Kocha Mkuu wa Azam FC amesema kuwa mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Simba utakuwa na presha kubwa ila ataingia uwanjani kama mechi za kawaida.

Lwandamina ambaye alichukua mikoba ya Aristica Cioaba ambaye alifutwa kazi siku moja baada ya kuboronga mbele ya timu ya Yanga amesema kuwa anatambua haitakuwa kazi nyepesi kuvaana na Simba.

Cioaba alifutwa kazi baada ya vinara wa Ligi Kuu Bara wakiwa na pointi 44 kumnyoosha kwa bao 1-0 kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Azam Complex na mabosi wa timu hiyo waliweka wazi kuwa hakuwa na mwendo mzuri ndani ya timu.

 

Februari 7, Lwandamina atakuwa na kazi ya kusaka pointi tatu muhimu mbele ya Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes ambaye amerithi mikoba ya Sven Vandenbroeck ambaye yupo ndani ya timu ya FAR Rabat.

Lwandamina amesema:-“Utakuwa mchezo mgumu ila tupo tayari kwa ajili ya ushindani na ninajua kwamba kila mmoja anafikiria juu ya presha hilo lipo wazi ikiwa unacheza na Simba ama Yanga.

Ni mchezo wa kawaida hivyo tutaingia ndani ya Uwanja kwa kujiamini na kujituma zaidi ili kupata ushindi,”.

Azam FC ipo nafasi ya tatu na pointi 32 baada ya kucheza mechi 17 inakutana na Simba iliyo nafasi ya pili na pointi 35.


TENGENEZA FAIDA KUPITIA KASINO YA MERIDIANBET

Neptune’s Richies ni mchezo Unaokupa pesa chap chap huku ukiwa unaburudika kupitia Kasino ya Mtandaoni ndani ya Meridianbet.

Neptune's-Riches_Casino-Post_30-January

Cheza hapa

10 Komentara

    Na wapambane kweli maana Simba wamejipanga sana

    Jibu

    Simba iko vizuri ila huu ni mpira lolote linaweza tokea

    Jibu

    Simba sio watu wa mchezo mchezo

    Jibu

    Pambaneni Paka FC

    Jibu

    Ngoja tuone mechi yenyewe itakuwaje siku hiyo

    Jibu

    Simba wako makini

    Jibu

    Simba nawakubali sana

    Jibu

    Fresh

    Jibu

    Ngoja tuone mpambano huo

    Jibu

    Kweli walipambana

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.