Christiano Ronaldo anajua kabisa kwamba hawezi kucheza soka kwa miaka mingine 20 lakini ameahidi kucheza kwa 100% kwa muda uliyosalia katika soka lake ikiwa amefikisha miaka 36 siku ya Ijumaa.
Mshindi huyo wa tuzo ya Ballon d’Or katika miaka 20 ya soka la kulipwa bado anakiwango thabiti na tayari amefunga magoli 22 na kutoa asisti 23 katika mshindano yote kwa Juventus msimu huu.

Nahodha huyo wa timu ya taifa ya Ureno katika siku yake ya kuzaliwa aliweka post katika akaunti yake ya Instagram, aliandika: “Miaka 36, Haiaminiki! nahisi kama imeanza jana, lakini safari hii tayari inahadithi na matukio lukuki ya kukumbukwa. Mpira wangu wa kwanza, timu yangu ya kwanza, bao langu la kwanza… muda unakimbia.
“Kutoka Madeira mpaka Lisbon,Lisbon mpaka Manchester, Manchester mpaka Madrid, Madrid mpaka Turin lakini juu ya yote kutoka kwenye moyo wangu. nimetoa kila kitu ambacho nilipaswa kutoa siwezi kurudi nyuma na kila wakati ninajaribu kutoa kilicho bora kadri ya uwezo wangu.
“Ikiwa nina sherehekea miaka 36 ya kuzaliwa na miaka 20 ya kazi yangu, nasikitika kusema siwezi kuahidi kucheza kwa miaka 20 mingine, lakini naweza kuahidi ilihali naendelea kusonga basi hutopokea si pungufu ya 100% kutoka kwangu.
“Asanteni kwa mara nyingine kwa sapoti yenu na jumbe zenu nzuri katika siku ya leo, hii inamaana kubwa kwangu wote mnanafasi maalumu katika moyo wangu.”
Neptune’s Richies ni mchezo Unaokupa pesa chap chap huku ukiwa unaburudika kupitia Kasino ya Mtandaoni ndani ya Meridianbet.



Sylvester
All the best Mwamba
Adelta
Good
Khadija
Safi sana cr7
Magdalena
Safi Ronaldo maana umri wenyewe unakutupa mkono
Caroline
Safi sanaaa Ronaldo
Dorophina
Ni Jambo jema alilosema mwamba
Sadick
Natarajia kuona CR7 akifikisha miaka 40 akiwa na uwezo wa kufunga magoli
Sarah
Safi sana
Hopemwaikuka
Gud
Lydia Emmanuel Magoti
Vizuri sana
Neema juma
Safi sana Ronaldo
warda
Kila la kheri kwake