Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Yanga SC mhandisi Eng.Hersi Said amesema hatua ya timu yao kupoteza mchezo dhidi ya Coastal Union ni muendelezo wa kutopata matokeo mazuri katika Uwanja wa CCM Mkwakwani.
“Haya matokeo sio mazuri kwetu lakini yanatupa nafasi ya kufahamu kwamba Uwanja wa Mkwakwani ni mgumu kwetu tunapoteza kwa miaka mingi sasa,” amesema Eng.Hersi.

“Kila Mwanayanga anatakiwa kutumia nafasi yake kutafakari ni wapi tunakosea kila tunapokuja sasa mkoani hapa, ilikuwa hivi pale Jamhuri Morogoro na tukabadilisha mambo msimu huu tuumize kichwa sasa na Mkwakwani.
Aidha Hersi amesema matokeo hayo pia yanatakiwa kufanyiwa tathimini kwa wachezaji wao ambapo watakutana nao mara baada ya kufika Arusha.
” Sio afya kuongea na wachezaji sasa baada ya matokeo haya lakini tutaongea nao tukifika Arusha kusikia wanakipi kilituangusha.“aliongeza Eng.Hersi
Ni Muda wa Kuvuna Mkwanja na Jungle Jim and the Lost Sphinx
Hauihitaji kufikira mara mbili ni mchezo gani utakupatia mkwanja ndani ya kasino za Meridianbet. Jiunge sasa ufurahie Jungle Jim and the Lost Sphinx.



Sadick
Hata hivyo Yanga imekuwa ikipata ushindi mwembamba tena kwa shida sana
Rahma
Yanga amna kitu
Sarah
Yanga kazi wanayo
Hopemwaikuka
Polen
Adelta
Yanga bado sana
Caroline
Yanga ipo juu
Mwanahamisi
Yanga baba lao
Venerose
Yanga mna tuangusha mashabiki wenu
Lydia Emmanuel Magoti
Pole yao
warda
Ndo mana wanatimuana