Nyota wa Liverpool Mohamed Salah amekuwa akihusishwa na kuondoka klabuni hapo. Kwa mujibu wa ripoti nchini Hispania, nyota huyu anajiandaa kuhamia Hispania wakati vilabu vya Barcelona na Real Madrid vikihusishwa naye zaidi.
Fowadi huyo alionekana kutokuwa na furaha baada ya kichapo cha bao moja bila dhidi ya Chelsea alhamisi, na taarifa zinasema Jurgen Klopp sasa anafanya jitihada kurejesha furaha yake kikosini hapo.

Salah alijiunga na Liverpool mwaka 2017 akitokea Roma kwa dau la £37.8m, hadi sasa nyota hiyu mwenye miaka 28 amecheka na nyavu mara 118 katika mechi 189 alizocheza tangia alipowasili klabuni hapo.
Alikuwa sehemu muhimu sana ya kikosi cha Liverpool katika kutwaa mataji ya Ligi Kuu Uingereza na Ligi ya Mabingwa Ulaya. Licha ya kuwa na mafanikio klabunia hapo, taarifa za kuhitaji kuondoka klabuni hapo zimekuwa zikichukua taswira kubwa zaidi.
Kwa mujibu wa ripoti za hivi karibuni, wakala wa staa huyu tayari ameshapanga mikutano na vilabu vyote viwili, Barcelona na Real Madrid, kipindi ambacho vilabu vyote viwili vikitajwa kuwa kwenye mawindo ya fowadi.
Ni Muda wa Kuvuna Mkwanja na Jungle Jim and the Lost Sphinx
Hauihitaji kufikira mara mbili ni mchezo gani utakupatia mkwanja ndani ya kasino za Meridianbet. Jiunge sasa ufurahie Jungle Jim and the Lost Sphinx.



Venerose
Mmmh kazi ipo
Adelta
Klopp yuko sahii kwenye mazungumzo yake
Hopemwaikuka
Atakavyo
Lydia Emmanuel Magoti
Ngoja tuone
Sarah
Maamuzi niyake
Caroline
Salah njoo madrid kwa wajanja
warda
Jamani salah si aje Man U