Mtu mmoja anaripotiwa kufariki dunia wakati wengine 39 wameumia katika uwanja wa taifa wa Madagaska kwenye mechi ya kufuzu michuano ya Mataifa ya Afrika AFCON 2019 kati ya Madagaska na Senegal ambayo iliisha kwa sare ya 2-2.
Shirika la habari la BBC linaripoti kuwa chanzo cha tukio hilo ni kusukumana na kukanyagana katika jitihada za kugombea kuingia uwanjani. Maelfu ya mashabiki walikuwa wakigombania kutumia lango moja ili kushuhudia mechi hiyo.
Watu wawili kati ya waliojeruhiwa wapo katika hali mbaya, makundi ya watu wengi yalianza kufika uwanjani mapema asubuhi kwa mechi inayochezwa saa 08:30 mchana kwenye uwanja huo wa Stade Municipal de Mahamasina.
Mechi hii iliwahusisha mastaa wakubwa kama staa wa Liverpool Sadio Mane, hawa ndio walivutia watu wengi zaidi kufika uwanjani hapo. Inadaiwa tatizo kama hili sio la kwanza kwa nchi za Afrika kufuatia kushindwa kuwa na mbinu mbadala ya kupunguza tatizo la idadi kubwa ya watu katika viwanja vidogo walivyonavyo. Hii inatakiwa kutumika kama funzo kwa nchi zingine za Afrika katika kuhakikisha usalama wa makundi ya watu wanaojitokeza kutazama mechi kama hizi.


Amani
Da hii sio poa aikuwa hali nzuri majeruhi waliku wengi ilipaswa mamlaka husika uwajibishwe
Povel
Duh polen sana